
Former Big Brother Africa housemates(BBA4),Kevin Chuwang Pam(from Nigeria) and Elizabeth Gupta(from Tanzania) who recently announced their engagement, are now about to move into the really thing;marriage.
According to a source close to the couple, they are planning to tie the knot this coming December in Nigeria.Kevin is expected to visit Tanzania sometimes soon to meet Elizabeth’s family and adhere some customs and traditions before the big day.
Kevin was the winner of BB4 and many Tanzanians still remember how he embraced the Tanzanian flag when he was declared a winner.

Jina la Sauda Mwilima (pichani)sio geni miongoni mwa watanzania wengi hususani wapenzi wa vipindi mbalimbali vya televisheni.Yeye ni mtangazaji kupitia Kituo Cha Televisheni cha Star kinachomilikiwa na kampuni ya Sahara Communications sambamba na vituo vya radio vya Kiss FM na Radio Free Africa.Vipindi anavyoruka navyo hewani ni Bongo Beats na Mcheza Kwao.
Hivi karibuni BC ilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano utakayoyasoma hivi punde.Je unajua Sauda anapendelea kuvaa namna gani anapotoka?Kuna mahali maalumu anapopenda kununulia “viwalo” vyake? Ana ushauri gani kwa vijana wengine ambao wangependa kuja kufanya kazi ya utangazaji kama yeye? Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC: Sauda,asante sana kwa kukubali kufanya nami mahojiano haya…mambo vipi?
SM: Mambo fresh tu.Nashukuru Mungu,siku zinakwenda.
BC: Kwa kuanza na kwa faida ya wasomaji wetu,unaweza kuniambia ulizaliwa lini,wapi,ukakulia wapi na mambo kama hayo?
SM: Nilizaliwa miaka 30 iliyopita,hapa hapa jijini Dar-es-salaam katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.Baadaye tulihamia Dodoma ambapo niliishi mpaka nilipomaliza elimu ya msingi ambapo nilirudi jijini Dar-es-salaam.Mpaka sasa maisha yanaendelea hapa hapa jijini Dar.
BC: Ilikuwaje ukaamua kufanya kazi ya utangazaji wa televisheni?Unaweza kukumbuka siku yako ya kwanza uliporekodi au kurusha kipindi cha televisheni “live”?
SM: Wakati nipo sekondari, ndoto yangu kubwa ilikuwa nikimaliza shule niwe Mwanasheria au Mwandishi wa Habari.Lakini baada ya kumaliza shule nikaangukia kwenye mambo ya habari. Na kikubwa zaidi nilivutiwa katika kazi ya utangazaji na dada yangu, Saida Mwilima, ambaye alikuwa mtangazaj TVT(Televisheni ya Taifa) ambayo kwa sasa inajulikana kama Tanzania Broadcasting Corporation (TBC). Nilivutiwa sana na kazi aliyokuwa akiifanya sister kwa sababu ni mtu ambaye nilikuwa naishi naye kipindi nasoma.Wakati huo yeye tayari alikuwa mtangazaji.
Yeah nakumbuka kipindi cha kwanza kwenda hewani ilikuwa mwishoni mwa mwaka 2004.Katika kipindi hicho niliwahoji AY,Ray C,Stara Thomas,Banana Zorro na Ruge Mutahaba. Hicho kilikuwa kipindi kimoja ambacho tulikuwa tunajadili kuhusu wasanii wa Kiume kuwapa support wa kike.Ruge nilimhoji katika nafasi ya Promoter anayechangia kukua kwa muziki.Hicho ndicho kilikuwa kipindi changu cha kwanza.
BC: Tuambie kidogo kuhusu kipindi chako pale Star TV.Maandalizi ya kipindi huwa yakoje na kwa mtu ambaye hajawahi kuangalia kipindi chako,nini maudhui ya kipindi?
SM: Star Tv nina vipindi viwili ambavyo nafanya kwa sasa. Cha kwanza kinaitwa Bongo Beats na cha pili kinaitwa Mcheza Kwao. Miaka miwili iliyopita niliwahi kufanya kipindi cha Afya.
Maandalizi ya kipindi ni kwamba kabla sijakutana na msanii husika kwanza huwa nafanya research(utafiti) kumhusu yeye kwa kutumia vyanzo mbalimbali. Kutokana na ninachokuwa nimepata kutoka kwenye utafiti,ndio naandaa maswali yangu. Kinachofuata baada ya hapo ni miadi ya kukutana katika location kwa ajili ya mahojiano. Kipindi cha Bongo Beats kinaruka hewani kila siku kasoro Jumapili tu. (more…)

Shindano la kumtafuta Bongo Star(mpya) katika muziki linaendelea. Shindano hilo lilianza tarehe 17 Julai na linaendelea mpaka tarehe 12 Agosti.Vipindi vya televisheni vitaanza kuonyeshwa kupitia Kituo cha Televisheni cha ITV kila Jumapili kuanzia tarehe 28 August mpaka mwisho wa shindano hilo.
Pichani ni majaji wa shindano hilo.Kutoka kushoto ni Espen Sorensen au maarufu kama Mzungu Kichaa. Yeye alizaliwa nchini Denmark na kisha akakulia Tanzania baada ya kuhamia hapa akiwa na miaka 6 kutokana na wazazi wake kuhamishiwa Tanzania kikazi.Ameshiriki katika harakati za muziki wa Hip Hop nchini Tanzania kwa muda mrefu.Hivi karibuni kwa kushirikiana na Proffessor Jay,alifyatua kibao Jitolee ambacho kilimweka katika chat za muziki kwa namna nyingine kabisa.
Katikati ni Rita Paulsen au Madame Rita kama anavyofahimika kwa wengi. Yeye ni Mkurugenzi wa Benchmark Productions ambao ndio waanzilishi wa shindano hilo.BC iliwahi kufanya naye mahojiano.Unaweza kuyasoma hapa.
Kulia mwa picha ni Joachim Kimaryo au maarufu kama Master Jay.Huyu ni Producer wa muda mrefu sana nchini Tanzania.Mwaka 1996 alianzisha studio ya MJ Records ambayo imekuwa chimbuko la wasanii wengi nchini Tanzania.

Washiriki wa shindano la mwaka huu la Big Brother Africa ndio wameanza kutajwa muda mfupi uliopita na Mwisho Mwampamba ambaye alishiriki shindano hilo mwaka 2003(Big Brother 1) na kuibuka mshindi wa pili ndiye mwakilishi wa Tanzania! Mwisho ndiye housemate wa kwanza kuingia ndani ya jumba la Big Brother.
Kwa ujumla washiriki wote wa mwaka huu,waliwahi kushiriki shindano hilo siku za nyuma na ndio maana limeitwa BBA All-star.Wengine waliorudi ni Paloma kutoka Zambia(Big Brother Africa 4),Jen kutoka Msumbiji(Mozambique) aliyeshiriki Big Brother Africa 4, Munya kutoka Zimbabwe(Big Brother Africa 4),Yacob kutoka Ethiopia(Big Brother Africa 4),Sheila kutoka Kenya(Big Brother Africa 3),Sammy kutoka Ghana(Big Brother Africa 1),Kaone kutoka Botswana(Big Brother Africa 4),Meryl kutoka Namibia(Big Brother Africa 2),Uti kutoka Nigeria(Big Brother Africa 3),Lerato kutoka South Africa(Big Brother Africa 2),Hannington kutoka Uganda(Big Brother Africa 4),Tatiana kutoka Angola(Big Brother Africa 2) na Code kutoka Malawi(Big Brother Africa 2)

Lile shindano maarufu la Big Brother Africa kwa mwaka huu wa 2010 linatarajiwa kuanza rasmi Jumapili ijayo yaani tarehe 18 Julai 2010 huko Johanesburg nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kampuni ya MultiChoice Tanzania, jumla ya washiriki 14 watatambulishwa siku hiyo wakati wakiingia katika Jumba la Big Brother. Shindano hilo litadumu kwa siku 91.
Mshindi wa Big Brother 2010 anatarajiwa kuondoka na kitita cha US Dollars 200,000. Kama kawaida shindano hilo litakuwa likirushwa hewani kupitia kituo cha DStv-Channel 198.
Tangu shindano hilo lianzishwe,kumekuwa na maoni tofauti tofauti kuhusu faida au hasara za shindano kama hilo.Wapo watu ambao wamekuwa wakidai kwamba shindano hilo linachangia katika kuporomoka kwa maadili kutokana na vitendo vya ki-ngono ngono vinavyofanywa na washiriki wa shindano hilo.
Pamoja na hayo,shindano hilo limekuwa likijipatia mashabiki na wafuasi chungu mbovu kila mwaka. Mwaka jana Tanzania iliwakilishwa na mmoja wa washiriki wa Miss Tanzania miaka ya nyuma, Elizabeth Gupta, ambaye alitokea kuwa miongoni mwa washiriki wenye mvuto katika jumba hilo.
Je ni nani ataiwakilisha Tanzania katika shindano la mwaka huu?Atakuwa wa jinsia gani? Stay tuned.


Anaitwa Irene Sporah Njau, ni mtangazaji wa Kipindi cha Sporah Show ambacho kinazidi kujipatia umaarufu na mashabiki.Lakini Sporah ni nani,ametokea wapi,ana malengo gani na ni kwanini anafanya anachokifanya? Ili kupata majibu ya maswali hayo na mengineyo bonyeza hapa kutembelea Spoti Starehe ili kucheki mahojiano kamili.

Yawezekana kabisa ukawa hufuatilii sana show ya Big Brother Africa ambapo watu fulani,wasichana kwa wavulana,huchaguliwa na kwenda kuishi ndani ya jumba moja(Big Brother House) kwa siku zisizopungua 90 huku kila kitu wanachokifanya ndani ya jumba hilo kikifuatiliwa,kurekodiwa na kuonekana kwa kila mwenye nia ya kuona kinachoendelea.
Sababu za kutofuatilia zinaweza kuwa nyingi.Unaweza kuwa huna muda.Unaweza kuwa huoni maana au mantiki ya kuketi mbele ya runinga yako na kutazama watu wengine huku ukitambua kwamba wanachokifanya pale ni kama mchezo wa kuigiza kitu ambacho hakibebi uhalisia.Mimi naamini kwamba wanapoanza ile show huwa wanaigiza.Lakini kadri mtu anavyozidi kukaa katika jumba lile,tabia au hulka yake ya kweli huibuka.Siamini kwamba mtu anaweza kuwa “fake” kwa siku zaidi ya 60!
Sababu za kuangalia pia zipo.Unajifunza mawili matatu.Unajifunza jinsi ya kuishi na watu,kuwasiliana na watu na pengine jinsi ambavyo mtu anaweza kunuia kufikisha ujumbe fulani kwa mwenzake au kwa jamii lakini akashindwa kueleweka au kutimiza lengo lake kutokana tu na uchaguzi mbovu wa maneno.Ukiiangalia show ile,unaweza pia kuona tofauti za kibinadamu miongoni mwa wanaume na wanawake.Sote tuna mahitaji sawa; kupenda,kupendwa,kuthaminiwa,kuheshimiwa nk lakini tuna njia tofauti tofauti za kufikia malengo yetu.
Lakini pia unaweza kujifunza kwamba unapomuona mtu kwa nje,usiwe mwepesi wa kudhani kwamba unamjua na unaelewa kila kitu alichopitia au anachopitia maishani mwake.Hili ndilo nililoliona baada ya kusikiliza ujumbe kutoka kwa binti anayeiwakilisha Tanzania(Elizabeth) katika show hiyo baada ya kutumiwa kipande cha video na msomaji mmoja wa BC.
Kwa wengi,Elizabeth ni binti mrembo mwenye kila nia ya kuendeleza sanaa ya urembo na uanamitindo.Utakumbuka kwamba aliwahi kuwania taji la Miss Tanzania bila mafanikio.Lakini je mambo ni safi au tambarare siku zote kwa Elizabeth? Anapitia au amepitia maswahibu gani maishani mwake? Msikilize Elizabeth katika kipande hiki cha video akiongea na wenzake.Bado huna sababu ya kumpigia kura za kubakia “mjengoni” Elizabeth?

Shindano la tatu la Big Brother Africa limemalizika leo huko Afrika Kusini ambapo kijana kutoka Angola, Ricardo David Ferreira Venancio a.k.a Ricco (21) kama alivyojulikana ndani ya Big Brother House ndio mshindi wa shindano la mwaka huu.
Tofauti na mashindano mengine,shindano la mwaka huu lilibidi liamuliwe kwa mbinde ya kutafuta asilimia ya jumla ya kura zote zilizopigwa mwaka huu baada ya Ricco kufungana na binti kutoka Malawi, Hazel(25)
Hongera kwa Angola kwa kuibuka washindi.

Kama kuna kitu ambacho kilitokea katika upande wa burudani nchini Tanzania hivi karibuni na kuteka hisia za watanzania wengi,bila shaka kitu hicho ni kundi lililokuwa linajulikana kama Ze Comedy.Tunasema lililokuwa linajulikana kama “Ze Comedy” kwa sababu mpaka sasa kuna utata au kesi kuhusiana na haki miliki ya jina hilo!Kesi iko kwa pilato.
Ilifikia kipindi ukimtafuta mtu siku ya Alhamisi jioni(wakati kipindi cha Ze Comedy kipo hewani) usipompata yawezekana kabisa yupo mbele ya luninga yake akiwacheki Ze Comedy huku simu yake akiwa ameiweka katika mtetemko(vibration) katika kumaanisha kwamba “hataki usumbufu”.
Wakati kundi hilo likizidi kujipatia umaarufu mara ghafla zikaja habari kwamba Ze Comedy wanakwenda “mapumzikoni”.Pamoja na kwamba tangazo hilo liliwasikitisha watu,ilieleweka kwamba mapumziko ni jambo muhimu kwa kila binadamu kwa hiyo watu wakaelewa!
Tatizo lilikuja pale mgogoro ulipofumka baina ya Ze Comedy na uongozi wa kituo cha EATV ambacho ndio kilikuwa kinarusha kipindi cha Ze Comedy kila siku ya Alhamisi saa moja jioni.Mapatano ya mezani yakashindikana.Kesi ikaenda mahakamani(bado ipo).Siasa nazo zikaingilia kati.Vigogo wa nchi wakaingilia lakini wapi.
Leo hii watu wengi wanajiuliza,je Ze Comedy watarudi? Na wakirudi watarudi kwa namna gani,kwa kutumia jina gani?Unadhani watakamata tena?Unadhani kilichotokea mpaka hivi sasa kinatoa mafunzo gani kwa vikundi vingine na washika dau wote wa fani ya burudani nchini Tanzania?
Kuna habari ambazo bado hazijaweza kuthibitishwa zinazosema kwamba vijana hao mahiri kwa kuvunja watu mbavu huku wakielimisha jamii wana mpango wa kufanya ziara kabambe nje ya Tanzania.Tunasubiri.

