TUZO ZA MUSEKE ONLINE AFRICA MUSIC AWARDS 2011

MWITO WA KUWASILISH


Museke, Inc. ina ufahari wa kutangaza kwa mwaka wa pili kutolewa kwa zawadi za Museke Online Africa Music Awards (MOAMAs), ambazo zitakamilika mwezi wa Septemba 2011. Wasanii, kampuni za kurekodi, maprodyusa na waakilishi wao wanaalikwa kujisajili kwenye vitengo kadhaa vilivyoko. Muziki ambazo zilitolewa na zimepata kuchezwa kwenye redio wakati wowote kuanzia Januari 1 2010 hadi 1 January 2011 zinastahiki kufikirika na kuingizwa kwenye shindano. Kwa mara nyingine, wapiga kura watatoka katika vitengo vinavyoheshimika katika nyanja za muziki, wakiwemo wana DJ. Kategoria zote za MOAMAs ziko wazi kwa wasanii wa Kiafrika walio na wasio kwenye bara. Wasanii wanaweza kuteuliwa kwa kupitia kiunganishi cha “nominate” kwenye tovuti
http://awards.museke.com.

“The Museke Online Africa Music Awards ni nafasi ya msanii wa Kiafrika kung’aa pasi na mipaka, nafasi ya kijishindia mashabiki zaidi. Mpango huu unakiri jukumu la mashabiki na wasanii la kuhakikisha uendelevu wa sekta ya muziki ya Kiafrika”, alisema Tumi Diseko, afisaa mkuu wa mauzo wa Museke.

Kama ambavyo Museke.com inavyozidi kukuwa na kupata umaarufu, nafasi mpya zinazidi kujitokeza: Museke.com kwa sasa iko katika mazungumzo na washika dau wengine kwa mkataba wa muda mrefu. Matokeo ya mazungumzo haya yatatangazwa baadaye.

Tuzo la Wapiga Kura
Hatimaye, washindi watachaguliwa kupitia kura – mashabiki ndiyo waamuzi wa kweli kwa tuzo za Museke Online Africa Music Awards. Ili kumpa motisha zaidi shabiki wa muziki za kiafrika, Museke iliamua kuanzisha tuzo la wapiga kura, Voter’s Choice Award, kitengo maalum ambacho kitashughulikia kazi ya wasanii wasiojulikana sana watakaojitokeza katika uteuzi wa MOAMA na muda wa kupiga kura utakaofuata.

read more

Zoezi la utoaji wa Kili Tanzania Music Awards lilipomalizika hapo juzi pale Diamond Jubilee Hall jijini Dar-es-salaam,jina moja lilibakia katika vinywa na bongo za mashabiki wa muziki na wote waliofuatilia tuzo hizo.Jina hilo sio lingine bali la Abbas Hamisi au maarufu kama kwa jina la kisanii la 20%.

Kijana huyo mzaliwa wa mkoa wa Pwani ambaye unaweza kusema bado ni msanii asiyejulikana sana hususani nje ya mipaka ya Tanzania,aliibuka “Mfalme” kwa kutwaa jumla ya tuzo 5 miongoni mwa vipengele 7 alivyokuwa ameteuliwa katika kuwania tuzo hizo. Kwa ujumla 20% aliibuka mshindi kama Male Artist of The Year(Msanii Bora wa Kiume), Best Male Singer(Mwimbaji Bora wa Kiume), Best Song Writer of The Year(Mwandishi Bora wa Nyimbo wa Mwaka) na huku kibao chake cha Tamaa Mbaya kikiibuka mshindi katika kipengele cha Best
Song of The Year(Wimbo Bora wa Mwaka) na Ya Nini Malumbano kikiibuka mshindi katika Best Afro Pop Song(Wimbo Bora wa Afro Pop).

Kwa bahati mbaya, 20% hakuwepo ukumbini kupokea tuzo zake na badala yake producer wake John Shariza “Man Water” kutoka Combinations Sounds ndiye alikuwa na kazi ya ziada ya kuzibeba tuzo 5 za 20%.

Kwanini yeye mwenyewe hakuwepo pale Diamond Jubilee Hall kupokea tuzo zile?Ni jinsi gani ameupokea ushindi huo? Kwanini anajiita 20%? Baada ya tuzo hizo,nini kinafuata katika maisha yake au kazi zake? Ili kupata majibu ya maswali hayo na mengineyo,BC ilimtafuta 20% .Fuatilia mahojiano yafuatayo;

BC: Mambo vipi 20%?

20%: Ee bwana mimi Mungu ananisaidia,sijui wewe brother.

BC: Yuko nasi pia.Kwanza hongera sana kwa ushindi wako wa juzi.Awards tano kwa mkupuo sio mchezo.Hongera sana

20%: Ni kweli kabisa Bro.Hata mimi namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kuibuka mshindi namna ile.

BC:Labda swali la kwanza ambalo watu wengi wangependa kujua ni ilikuwaje ukakosa kuhudhuria shughuli ya utoaji wa tuzo zile? Nini kilitokea?

read more

Mwanaidi Hassan,akilia kilio cha furaha na kutoamini alipotangazwa kuwa Mwanamichezo Bora nchini Tanzania kwa mwaka uliopita wa 2009.Mwanaidi anacheza mchezo wa Netball.Anachezea timu ya JKT Mbweni na Timu ya Taifa ya Netball.Utoaji wa tuzo hizo ulifanyikia New Africa Hotel jijini Dar-es-salaam.

Mwanaidi Hassan(katikati) akikabidhiwa Tuzo ya Uanamichezo Bora na kitita cha shilingi Milioni Moja(1m Tshs).Anayemkabidhi ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania(BMT),Kanali Iddi Kipingu.Wanaoshuhudia pembeni,kutoka kulia kwenda kushoto ni David Nyombo,aliyechukua Ushindi wa Tatu kupitia mchezo wa kunyanyua vyuma vizito(body building),Juma Kaseja,aliyechukua ushindi wa pili kupitia mchezo wa Soka.Kaseja ni golikipa wa Simba Sports Club ya jijini Dar-es-salaam.Mwingine pichani ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo(TASWA),Boniface Wambura.TASWA ndio waandaji wa tuzo hizo.

Juma Kaseja(kulia) akipokea Tuzo ya ushindi wa pili.Kaseja, golikipa nambari moja wa Simba.Anayemkabidhi ni Jaji Mark Bomani,Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tuzo hizo.

David Nyombo,mnyanyua vyuma vizito,akikabidhiwa tuzo yake ya ushindi wa tatu.

Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini na wadau wa TASWA.

Picha zote na Richard Mwaikenda.

Imeandikwa na Na Angela Semaya wa Habari Leo

MAISHA yake sasa yamebadilika, amelazimika kuwa mtumwa wa kujificha kwa kuvaa vazi aina la Hijab ambalo anasema kwake limegeuka kuwa vazi analoliheshimu na kulithamini kwa kuwa ndio msiri wake mkubwa siku hizi, hii yote ni gharama inayotokana na moyo wake wa ujasiri na ushupavu uliotokana na kutumia kalamu yake kufichua uovu na unyanyasaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kuuawa kwa imani za kishirikina.

Kwa walio wengi ndani na nje ya Tanzania, jina la Vicky Ntetema sio geni masikioni mwao kwani ni mwandishi mahiri wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Ntetema aliyezaliwa miaka 51 iliyopita ameibuka kuwa mwandishi mahiri, jasiri na shupavu baada ya kufichua siri ya kutisha kutokana na uchunguzi wa mauaji ya albino na familia zao akitaka kujua kwa undani sababu hasa za mauaji na ukatili dhidi ya albino. Hatimaye kazi yake hiyo imemuwezesha kupata Tuzo ya Ujasiri katika fani ya Uandishi wa Habari inayotolewa na International Women’s Media Foundation.

HABARI LEO Jumapili iliamua kumtafuta Vicky baada kutaka kufahamu kwa undani wa kilichomsukuma kufuatilia habari hiyo na kwa kiwango gani amefanikiwa, maisha yake kwa ujumla na kuhusiana na tuzo hiyo.

Ntetema ambaye alifanya uchunguzi wake kwa siri bila woga anasema Novemba, 2007 alipokea ujumbe wa maneno ukimuelezea kuhusu matukio ya kuuawa albino na kukatwa viungo vyao kwa imani za kishirikina, lakini awali naye hakuamini kama hicho kitu kinawezekana.

Na baada ya kufuatilia kwa muda na kujithibitishia habari hizo, alianza kuishawishi BBC, lakini walionekana kusitika wakiwa na mashaka kwamba kweli inawezekana kuwepo kwa matukio hayo? Hata hivyo anasema hakukata tamaa aliwasiliana na waandishi wengine walioko katika maeneo husika nao walimsaidia kuchunguza na kumpa taarifa zaidi.

Wakati akiendelea na uchunguzi wake aligundua kuwa waganga wa kienyeji ndio waliokuwa wakisababisha mauaji ya albino kwa kuwaambia wateja kuwa wanaweza kupata utajiri kwa kutumia viungo vya walemavu hao, ndipo alipoamua kuishawishi tena BBC huku akiendelea na uchunguzi wake kwa njia ya simu kwa kuwasiliana na watu wa Kanda ya Ziwa.

Kile alichokuwa amekusudia kukifanya na kukifichua, kilithibitishwa na Rais Jakaya Kikwete ambaye Mwezi Machi, 2008 alikemea vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya albino na kuweka wazi kuwa tayari watu 19 walishauawa.

“Baada ya Rais kutangaza hivyo, nikasema kama kiongozi wa nchi amekemea kiasi hili na ametaja hadi maeneo yanayohusika na matukio hayo…kwa sababu ya kuwa na uhusiano mzuri na wahariri nilipeleka maombi yangu bila kusita wanisaidie ili niweze kwenda kabisa eneo husika ingawa waliniambia kwa kipindi hicho hawakuwa na bajeti,” anasema.

Dhamira yake ilimsukuma Ntetema kuchukua fedha zake za mshahara na kuamua kwenda Mwanza kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi wake. Anasema kazi hiyo ilimlazimu kuzunguka sehemu mbalimbali hadi akajikuta ameishiwa fedha na kulazimika kuomba kwa mama yake. read more

aybcshaa

AFRICAN MUSICIANS BATTLE IT OUT FOR THE 2009 MTV AFRICA MUSIC AWARDS WITH ZAIN

Nairobi, 25 August 2009: MTV and Zain have disclosed the contenders for the 2009 MTV Africa Music Awards with Zain, the global celebration of African contemporary music talent and youth culture. The nominees, from across the Continent’s contemporary music spectrum, were revealed by Alex Okosi, Senior Vice President & Managing Director, MTV Networks Africa and Mwambu Wanendeya, Zain Group Communications Director – Africa, at a star-studded bash at The Loft in Nairobi, Kenya.

The big names in African music are ready to do battle as South African, Nigerian and Kenyan artists make a big impact among the nominations for the 2009 MTV Africa Music Awards with Zain. South Africa and Nigerian artists received an incredible 15 nominations while Kenya achieved 6 nominations – the best tally yet for the East African nation and host country for the upcoming 2009 event!

Nigerian music royalty and R&B superstar 2FACE achieved the highest number of nods from the MAMA academy including nominations for Best Male, Artist of the Year, Best Video and Best R&B. Hot on his heels were South Africa’s HHP, Kenya’s Nameless and fellow Nigerian D’Banj – who are each nominated in three categories.

South Africa Afro Soul goddess Lira, who is scheduled to perform at the awards, topped the list of female nominees, earning two nods for Best Female and Artist of the Year. Other contenders in a strong Best Female line-up include Kel (Nigeria), Amani (Kenya), Zamajobe (South Africa) and Lizha James (Mozambique).

Uganda and Tanzania made a strong showing, contributing 5 nominations between them including two accolades for Ugandan female trio Blu*3 (Best Performer, Best Group) and a Best Video nomination for XOD – I Want You Back. Tanzanian artists were recognised in two categories including Best New Act (Shaa) and Best Hip Hop (A.Y.). Ghanaian star Samini is a hot contender in the Best Performer category after narrowly missing out to Jozi in the Best Live category in the 2008 Awards. read more

Muite Steven Kanumba.Hapa ilikuwa wiki iliyopita wakati wa utoaji wa tuzo za Vinara wa filamu Tanzania. Waandaaji wa tuzo hizo walimpa Kanumba Tuzo ya Heshima kutokana na mchango wake katika maendeleo ya filamu nchini Tanzania.Kuna watu wanakubaliana na uamuzi huo wa waandaaji wa tuzo hizo na kuna ambao hawakubaliani wakisema kwamba ni mapema mno kwa Kanumba kupewa “tuzo ya heshima”.Wewe unasemaje?

Mwingine aliyepewa tuzo ya heshima ni Ngumbagwe Misayo au maarufu kama Thea.Ukitaka kusoma mahojiano tuliyowahi kufanya na Steven Kanumba siku za nyuma,bonyeza hapa.

Photo/A.Mrisho

Ijumaa iliyopita ilikuwa ndio siku Tuzo za Vinara zilipokabidhiwa. Kwa maana hiyo historia mpya imeandikwa ingawa ni wazi kwamba kazi kubwa bado iko mbeleni kama ni kweli kuna dhamira ya kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia kwa upande wa filamu na maigizo. Kwa wale ambao mngependa kujua, hii hapa ndio orodha kamili ya waliokuwa wameingia fainali za kuwania tuzo hizo(na vipengele walivyokuwa wanawania) na majina ya washindi yakiwa yanajionyesha.

Pichani ni washindi wa tuzo hizo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi,Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo,Joel Bendera. Kwa picha zaidi kuhusu tukio hili mtembelee Ahmad Michuzi wa Jiachie.

WASHINDI WA TUZO ZA VINARA WA FILAMU TANZANIA

Mapambo na Maleba

Misukosuko 2

Macho Mekundu

Kolelo (mshindi)

Utata

Copy

Mnasa Sauti Bora

Adam Waziri (Fungu la Kukosa)

Creophance Ng’atingwa (Kolelo)-mshindi

David Sagala (Copy)

Camillius Kamili (Fake Pastors)

Swaleh Juma (Misukosuko 2) read more

 

Sherehe za kumtangaza Mwanamichezo Bora wa Mwaka 2007 nchini Tanzania zinatarajiwa kufanyika ijumaa hii kwenye ukumbi wa Landmark,Ubungo jijini Dar-es-salaam.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Kiongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha.Ni kina nani wanawania tuzo hiyo muhimu kwa wanamichezo?Bonyeza hapa kupata jibu.

Pichani ni mwanamichezo bora anayemaliza muda wake,mwanariadha Samson Ramadhani, mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za marathoni kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka juzi huko jijini Melbourne nchini Australia.

 

Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amepokea rasmi tuzo inayoheshimika ya Martin Luther King. Mengi anakuwa Mtanzania wa nane kutwaa tuzo hiyo. Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.BC inampongeza Mengi kwa tuzo hiyo.

 

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Banana Zorro(kushoto) na Ray C(kulia) baada ya kutwaa tuzo za Kili Music Awards mwanzoni mwanzoni mwa mwaka huu (2007) unaoelekea ukingoni. Ray C alishinda tuzo ya Best Female Vocalist of the Year(mwimbaji bora wa kike) wakati Banana Zorro alishinda tuzo ya Best Male Vocalist of the Year (mwimbaji bora wa kiume) na hivyo kuwa msanii wa kwanza kutoka kwenye muziki ujulikanao kama Bongo Flava kushinda tuzo hiyo.Siku za nyuma tuzo hiyo imekuwa ikinyakuliwa na waimbaji wa bendi zaidi.

Tunapoelekea kuuaga mwaka wa 2007 BC itakuwa inakupa kumbukumbu za hapa na pale za matukio yaliyojiri mwaka huu wa 2007.

↑ Go Back to Top of Page