
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,akila kiapo kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania,Augustino Ramadhan.Sherehe hizo zimefanyika mapema leo katika Uwanja wa Uhuru(Uwanja wa Taifa) jijini Dar-es-salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali barani Afrika bila kuwasahau wakazi wa jijini Dar-es-salaam na mikoa ya jirani.

Hatimaye Tume ya Uchaguzi Tanzania,imetangaza rasmi matokeo ya Kura za Uchaguzi wa nafasi ya Urais.Katika matokeo hayo,Rais Jakaya Mrisho Kikwete,ameshinda kwa kiwango cha asilimia 61.17%. Katika uchaguzi wa mwaka 2005, Rais Kikwete alipata ushindi wa asilimia 80.28%. Matokeo kamili ni kama yafuatayo;
1. KUGA PETER MZIRAY APPT – MAENDELEO 1.12%
2. KIKWETE JAKAYA MRISHO/CCM – 5,276,827 61.17%
3. SLAA WILLIBROD PETER/CHADEMA – 2,271,942 26.34%
4. LIPUMBA IBRAHIM HARUNA/CUF – 695,667 8%
5. RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 26,388 0.31%
6. MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 17,482 0.20%
7. DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 13,176 0.15%

Aliyekuwa Mgombea wa Kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),Dr.Wilbrod Slaa, leo hii amejitokeza na kuongea na baadhi ya vyombo vya habari na kuelezea mapungufu,shaka za uchakachuaji wa kura na pia kutoa mapendekezo yake juu ya nini kifanyike au kifanywe na Tume ya Uchaguzi Tanzania(NEC).
Miongoni mwa vyombo vya habari alivyoongea navyo,ni pamoja na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya America(VOA). Msikilize kwa kubonyeza player hapo chini akiongea na mtangazaji Sunday Shomari, wa Idhaa hiyo.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Kwa habari zaidi unaweza kutembelea Ukurasa wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika(VOA).

Gazeti la Mwananchi limefanya jambo moja muhimu sana.Limeorodhesha ahadi ambazo wagombea Urais wamekuwa wakizitoa kwa wapiga kura katika nyakati mbalimbali za kampeni.
BONYEZA HAPA KUZISOMA AHADI ZENYEWE. Kwa yeyote atakayeshinda kiti cha Urais(bado hatujajua mshindi wa kiti cha Urais mpaka jamaa wa Tume ya Uchaguzi watakapopenda kutoa matokeo!),ahadi hizi ndizo zitatumika kuona ni jinsi gani wanasiasa ni watu wa kuaminika au kutoaminika.
…ONE CAN SAY YES AND THE OTHER ONE CAN SAY NO…AND BOTH CAN BE RIGHT AND PEACEFUL…

Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA,Dr.Wilbroad Slaa,akimnadi mgombea ubunge katika Jimbo la Ubungo kupitia chama hicho,John Mnyika.Wapiga kura wengi bila shaka walikubaliana na ombi la Dr.Slaa kwa kumchagua Mnyika kuwa mbunge wao mpya.

JK alipokuwa akimnadi Basil Mramba aliyekuwa mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro.Kwa bahati nzuri au mbaya,wapiga kura walikuwa na mtazamo tofauti.

Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA,Dr.Wilbroad Slaa,akimnadi mgombea Ubunge kupitia chama hicho katika Jimbo la Karatu,Mchungaji Israel Natse.Wapiga kura jimboni hapo waliafikiana na Dr.Slaa na kumchagua Mch.Natse kuwa Mbunge wao mpya.

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Jakaya Kikwete,akimnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza,Lawrence Masha.Huko nako wapiga kura walikuwa na mtazamo tofauti.Demokrasia ikaamua.

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete,akimnadi mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza,Anthony Diallo.Wapiga kura walikuwa na mrengo tofauti.

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Jakaya Mrisho Kikwete,akimnadi mgombea Ubunge kupitia tiketi ya chama hicho katika Jimbo la Monduli,aliyewahi kuwa Waziri Mkuu,Edward Lowassa.Wapiga kura wa jimbo hilo walikubaliana na ombi la Jakaya Kikwete kwa kumrudisha bungeni Mh.Lowassa.

Halima James Mdee-Mshindi Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA.

January Makamba-Mshindi Jimbo la Bumbuli kwa tiketi ya CCM

John Mnyika- Mshindi Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA

Peter Serukamba-Mshindi Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya CCM

Zitto Zuberi Kabwe-Mshindi Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA
More to come…stay tuned!

Wapo watu wengi,hususani vijana, ambao BC inawapongeza na kadiri siku zinavyokwenda,itazidi kuwapongeza kwa ushindi waliojinyakulia wakati wa kuwania nafasi za kuwawakilisha wananchi hao katika Bunge na pia kuwaongoza wananchi katika harakati za kujiletea maendeleo.
Kwa leo,tunadhani sio mbaya tukaanza kwa kumpongeza Mr.Joseph Mbilinyi a.k.a SUGU. Ukiwa huna hiana, unaweza kuanza kumuita Mheshimiwa Joseph Mbilinyi.Hongera sana.
Tunapompongeza,sio vibaya pia kukumbushana enzi zile(sina uhakika bado kama ataziacha kwa kuwa sasa ni mwendo wa tai na suti). Hapa chini ni wimbo wa “Mheshimiwa” uliokwenda kwa jina Sugu akiwa amemshirikisha Stara Thomas.Msikilize.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar,imemtangaza Dr.Ali Mohamed Ali Shein, kuwa mshindi wa kiti cha Urais upande wa visiwani Zanzibar.
KURA HALALI ni 358,815
KURA ZILIZOHARIBIKA ni 6109
DK ALI MOHAMMED SHEIN (CCM) amepata 179,809 sawa na 50.1%
MAALIM SEIF SHARIF HAMAD (CUF) amepata 176,338 sawa na 49.1%
SAID SOUD SAID amepata 480
KASSIM ALI BAKARI amepata 803
HAJI AMBAR KHAMIS amepata 363
HAJI KHAMIS HAJIamepata 525
JUMA ALI KHATIB amepata 497

Naomba niweke jambo moja wazi.Tume ya Uchaguzi Tanzania au The National Electoral Commission(NEC) inakatisha tamaa.Kama kuna mahali ambapo nilitegemea pawe na matokeo ya Uchaguzi wa mwaka huu wa 2010 ya uhakika,basi mahali hapo ni kwenye tovuti rasmi ya Tume ya Uchaguzi.
Tofauti na matarajio hayo,tovuti hiyo inaonekana ipo usingizini kabisa.Hakuna matokeo yoyote au habari zozote za maana kuhusu Uchaguzi uliofanyika jana.Kipo kichwa cha habari kwamba Tume yaanza kutangaza matokeo ya awali ya Urais.Hakuna content yeyote ndani ya kichwa hicho cha habari.Na hii wameitoa kama Breaking News!
Hivi kuna ugumu gani au inahitaji watu wangapi kuifanyia updates tovuti hiyo?Nilidhani kutokana na umuhimu wa zoezi kama la Uchaguzi,basi tume hiyo ingekuwa na watu kadhaa,wataalamu wa masuala ya tekinolojia ya mtandao ili kuhakikisha kwamba wanakuwa na up to minute news.Mwananchi anapokosa imani ya tume hii,utamlaumu?Get serious tume.
ILI KUPATA MATOKEO NA MATUKIO YANAYOJIRI KUHUSIANA NA UCHAGUZI WA MWAKA HUU TEMBELEA TOVUTI NA VIUNGANISHI VIFUATAVYO;
Tanzania Broadcasting Corporation(TBC)
Na pia unaweza kuangalia kupitia blogs mbalimbali.Chungulia hapo kushoto mwa ukurasa huu na bonyeza Blogroll


sending...