Ingawa kila siku idadi ya bloggers wa kitanzania inazidi kuongezeka,idadi ya wanawake wanaoblog bado ni ndogo ikilinganishwa na wale wa kiume.Yawezekana ni kwa sababu wanawake bado hawajapata mwamko wa kutosha au pengine ni kitu ambacho bado wanakipa kisogo.

Lakini pamoja na idadi ya wanawake kuwa ndogo,wanaofanya hivyo wanafanya kazi nzuri sana ya kuwawakilisha wanawake wenzao.Miongoni mwa wanawake hao ni pamoja na Shamim Mwasha au Zeze kama anavyojulikana kwa watu wake wa karibu.

Iwe ni shughuli yenye mvuto wa kitaifa au wa mtu binafsi(hususani zile zenye kuwagusa wanawake zaidi),ukihudhuria na kutizamatizama katika watu waliopo mstari wa mbele katika kuchukua kumbukumbu iwe ni kwa kutumia picha za mgando(still photos) au videos,bila shaka waweza kumuona Zeze.Ukimsalimia atakujibu na kukurushia tabasamu ambalo naweza kusema ni “signature” yake.

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ambayo utayasoma hivi punde.Zeze ambaye blog yake inakwenda kwa jina www.8020fashions.blogspot.com, anaweka bayana mambo kadhaa kuhusu harakati zake kama mwandishi wa habari(taaluma yake) na pia blogger pamoja na ujasiriamali.

Yote tisa,kumi ni kwamba siku chache zijazo,Shamim kupitia blog yake ya 8020fashions,anasheherekea miaka mitano(5) tangu aanze shughuli ya kublog au Libeneke la kublog kama ambavyo rafiki yangu Issa Michuzi hupenda kuiita shughuli hii.Nimemuuliza pia maswali machache kuhusu siku hiyo maalum kwake na kwa wapenzi wa blog yake ambayo itafanyika pale Diamond Jubilee tarehe 30 October,2011.Twende pamoja katika mahojiano yafuatayo;

BC: Umekuwa uki-blog kwa muda gani mpaka hivi sasa?Nini kilikusukuma katika kuanzisha blog yako?

SM: Huu ni mwaka wangu wa tano sasa tangu nianze hili libeneke.Kikubwa kilichonisukuma kilikuwa ni nia yangu ya kutangaza biashara ya duka langu la nguo liitwalo 8020 Fashion lililopo Sinza.Nikaona nifungue blog ili niwe naweka nguo na bidhaa zingine kadiri zinavyowasili dukani.Sasa kama ujuavyo si kila siku naweza kuwa na new arrival na ili watu warejee kuangalia blog ndio nikaanza kuweka picha za matukio mbalimbali huku nikiwa nimejikita kwenye fashion zaidi katika kuonyesha nini kilivaliwa wapi na nani na mambo kama hayo.

BC: Kitaaluma wewe ni mwandishi wa habari. Sasa ukiwa kama blogger,unadhani kuna tofauti gani za kimsingi kati ya mwandishi wa habari wa kawaida na blogger? Je,kuna misingi ambayo wote (a journalist and a blogger) wanayotakiwa kuzingatia?

SM: Ni kweli kabisa,ipo tofauti kubwa sana. Kama ujuavyo blogger inakuwa ni mimi kama mimi ambapo nisipo-update ni blog inakuwa imelala doro. Hivyo kuwa kama blogger inabidi uwe na juhudi binafsi za kujituma kitu ambacho ni tofauti na mwandishi wa habari ambapo hata wewe usipoenda kazini au kufanya kazi gazeti ni lazima litoke tu.

BC: Blog yako imejikita zaidi katika kuandika habari za urembo,shughuli kama vile harusi,kitchen party,fashion shows nk.Ni kwanini uliamua kuwa na “niche” kama hiyo?

read more

If you try to dig the history books of the Tanzanian world of Fashion and Beauty, you will most likely come across the name Linda Bezuidenhout. She is one of first enthusiasts of fashion and beauty in Tanzania. I am talking about the  days when she owned a once most famous beauty salon in Dar-es-salaam(Lamia Salon) to the days when she used to be the official beautician  for the beauties of Miss Tanzania Beauty Pageant.

Married with three kids,she now lives in Georgia,USA where she continues to follow her passion of fashion,clothing and beauty in a little bit different way.She is now an even more serious entrepreneur.She recently caught up with our sisters of Fashion Junkii for a candid interview. Click here to read it all.

dk-kyaruzi-at-college-3bc

Na Freddy Macha

Mwezi jana tulitoa sehemu ya kwanza ya mahojiano na mmoja wa wataalamu na wasomi wetu mkazi na mhadhiri anayeishi Uingereza Dk. Imani Silver Kyaruzi. Kitabu chake mkakata “Mbinu za Ujasiriamali” kitasaidia sana kuendeleza uchumi na akili za Mtanzania hasa yule anayependa kujiendeleza au kufanya biashara. Kilichapwa na “Mkuki Na Nyota” mjini Dar Es Salaam mwaka jana.

FM: Turudi katika uandishi Tanzania. Mkuki na Nyota ni wachapishaji pekee wanaowakilishwa kidogo nje, wenye tovuti na wanaojitahidi. Je kitabu kinauzwa vizuri? Ulichapisha nakala ngapi? Je, wasomaji wengi wako nje au ndani? Unayo njia ya kuyajua hayo?Unaridhishwaje na hali ya uandishi na usomaji wa vitabu nchini.

Dk. Imani Kyaruzi: Mkuki na Nyota wanao mpango wa kukiendeleza na kukisambaza kitabu hiki nchini kote. Kazi hii imeanza tayari na ninategemea mawasiliano hivi karibuni. Nakala zilizochapishwa ziko katika maelfu na ninaweza tu kuongelea wanunuzi wa bara la Ulaya. Wakati wa unzinduzi nilifanikiwa kusaini nakala nyingi sana na kitabu kilipokelewa vizuri na umati wa Watanzania waishio Uingereza. Baadhi ya nakala zilienda Ujerumani kwa wasomaji wa huko na marejesho yanaridhisha.

Nia ni kuwafikia wasomaji wa ndani na kazi hii itaanza baada ya majuma mawili. Ningependa kutoa mafunzo nyumbani wakati wa kukitangaza kitabu hiki.

Kuhusu uandishi na usomaji, inasikitisha sana kwani tumezoea kuona vitabu vya kina Michael Porter na kina Mr Smith na ninafikiri Watanzania tukianza kuandika italeta changamoto kwa waandishi walioko nyumbani ambao naamini wako wengi, tu. Kwa upande wa usomaji sina uhakika na hilo, ila tu ningependa kusisitiza kuwa vitabu vya mitaala hadi Chuo Kikuu viwakilishwe na vitabu vilivyoandikwa na wazalendo na vyenye kulenga katika hali halisi ya nchi. Hii ni muhimu kwani vitabu vyenye maudhui ya Kiulaya vinawatayarisha vijana wetu kutumikia nchi gani? read more

Mwaka jana mmoja wa wataalamu na wasomi wetu mhadhiri anayeishi Uingereza Dk. Imani Silver Kyaruzi alitoa kitabu moto moto “Mbinu za Ujasiriamali” kitakachosaidia sana uchumi na akili za Mtanzania hasa yule anayependa kujiendeleza au kufanya biashara. Kitabu hiki kilichochapishwa na “Mkuki Na Nyota” mjini Dar Es Salaam ni kidogo chenye kurasa 50. Hivi karibuni alifanya mahojiano na Freddy Macha. Hii ni sehemu ya Kwanza ya mahojiano hayo.

dr-kyaruzi-na-susan-mzeebc

Dr.Kyaruzi(kulia) akiwa na Katibu Wa Chama cha Watanzania nchini Uingereza,Suzan Mzee(kushoto) wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho Birmingham-October 2008.

FM :Muundo au fani yako ni kuuliza maswali na kupanga vichwa rahisi vya kuelewa kimaneno. (“Je wewe unauza nini?” ” Je unahitaji watu wa kushirikiana nao?”).

Twaweza kusema kazi yako ya kufundisha (Mhadhiri, Uingereza) imeathiri muundo wa kuandika kitabu hiki kizuri chenye lugha nyepesi kueleweka?

 

Dk. Imani Kyaruzi: Kweli kabisa…niliamua kutumia lugha nyepesi na yenye kueleweka baada ya kugundua kuwa watu wengi (wafanyabiashara) wanashindwa kufuatilia maelezo yaliyomo katika vitabu vya kimataifa vya ujasiriamali. Si Tanzania tu, bali hata hapa Ulaya wafanyabiashara hawana muda wa kusoma madoido ya kisomi yasiyoeleweka! Ila kwa upande mmoja haikuwa rahisi kuandika kitabu hiki kwa lugha kiswahili kwani nina muda mrefu tangu nimeondoka Tanzania na lugha imebadilika sana. Utakuta katika baadhi ya maneno nimejaribu kufikiri katika lugha zote mbili na kutafuta maneno yatakayofaa kuufikisha ujumbe bila kuupotosha. read more

Mara moja moja huwa inatokea celebrities wa Bongo wakakutana.Hali hiyo ikitokea huwa ni wakati muafaka wa kubadilishana mawazo na kupiga picha kama inavyoonekana hapa.Pichani kutoka kushoto ni Rita Paulsen,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Benchmark Productions,Mfanyabiashara maarufu,Kinje na K-Lyinn,mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya na pia Miss Tanzania mwaka 2000.Picha ya zamani kidogo hii.

Kwa wengine bado anaendelea kuwa mchora katuni aliye maarufu zaidi nchini Tanzania.Kwa wengine ni mtangazaji maarufu wa redioni ambaye kila asubuhi huwapa wasikilizaji habari mbalimbali na pia burudani. Lakini kwa wengine,yeye ni mbunifu wa mitindo(fashion designer) ambaye anakuja juu kwa kasi ya aina yake.Huyu si mwingine bali Ali Masoud,(pichani) maarufu kama Masoud Kipanya au ukipenda KP.

Leo hii yawezekana kabisa kusema kwamba Masoud ni kijana mjasiriamali ambaye anajaribu kutizama mbali kushinda maelezo. Ni kijana anayependa kujishughulisha kwa bidii na maarifa bila kuchoka wala kukata tamaa.Mwaka jana alitimiza mojawapo ya ndoto zake za muda mrefu kwa kuzindua lebo/nembo ya KP iliyokwenda sambamba na KP Wear.Hivi leo sio ajabu kukutana na watu mitaani waliovalia nguo zenye nembo na ubunifu kutoka kwa KP!

Kwa mara ya pili,hivi karibuni BC ilifanikiwa kupata fursa ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na sio uchoraji katuni wala utangazaji bali ubunifu wa mitindo. Nini kilimsukuma kuingia kwenye fani ya ubunifu wa mitindo?Unataka kuijua falsafa inayomuongoza katika fani hii?Je anahofia kitu gani zaidi linapokuja suala zima la ubunifu wa mitindo?Nini mipango yake ya sasa na baadaye kidogo?Kwa hayo na mengineyo mengi zikiwemo picha za baadhi tu ya viwalo vilivyosheheni ubunifu wake,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; read more

 

Asha Baraka (kulia)Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET) ambao ndio wamiliki wa bendi mbili za muziki wa dansi zinazotamba nchini; The African Stars Twanga Pepeta International na The African Stars Twanga Chipolopolo akiteta jambo na Mbunge wa Ilala,Mheshimiwa Mussa Azan Zungu. Asha Baraka hujulikana pia kwa jina la “Iron Lady”.

BC ipo mbioni kufanya mahojiano na Asha Baraka ambaye inaaminika ndio mwanamke pekee nchini Tanzania ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza vipaji vya wasanii mbalimbali sambamba na uwezo wa hali ya juu wa kuziendesha bendi za muziki kitu ambacho sio rahisi.

 

Baadhi ya mitindo kutoka kwa Masoud Kipanya au KP.Kwa habari zaidi unaweza kutembelea www.kpwear.com.

Kila mwaka,tarehe 14 February(Siku ya Wapendanao),yeye hukumbuka au kusheherekea siku yake ya kuzaliwa. Alipozaliwa wazazi wake walimuita Fina.Leo hii wengi tunamfahamu kama Fina Mango(pichani),mtangazaji maarufu wa kituo cha radio cha Clouds FM.

Yeye ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watano(5) kwa upande wa mama yake, Fortunata M.Mango na watoto saba(7) kwa upande wa Marehemu baba yake,,Joseph Mango.Anaye dada mmoja na kaka watatu(3) wa kuzaliwa tumbo moja na dada mmoja na kaka mmoja wa kambo.

Alianza pilikapilika za masuala ya elimu mkoani Arusha katika shule ya Mtakatifu Constantine(St.Constantine) na baadaye kujiunga na shule ya sekondari Jitegemee jijini Dar-es-salaam kwa ajili ya masomo ya O-Level.Kisha akajiunga na shule ya Shaaban Robert ya jijini Dar-es-salaam kwa masomo ya A-Level na kuhitimu mwaka 1999. Baada ya hapo akajiunga na Clouds FM ingawa kimasomo hakuishia hapo kwani baadaye alijiunga na FTC(Financial Training Centre) ambapo amesomea masuala ya biashara.Bado ana mpango wa kuendelea zaidi kimasomo.

Leo hii yeye ni Brand Manager wa kipindi cha Power Breakfast ambacho anakiendesha kwa kushirikiana na Masoud Kipanya (KP).Kipindi kinarushwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12 alfajiri mpaka saa 3 asubuhi.

Fina Mango pia ni mjasiriamali, yeye ndio mmiliki wa kampuni ijulikanayo kama One Plus Communication ambayo inashughulika na masuala ya Usimamizi wa Shughuli na Matukio ya Mashirika mbalimbali na Uhusiano wa Jamii (Corporate Events Management & Public Relations (PR). Ofisi za One Plus Communication zipo maeneo ya Victoria ilipo Victoria Gas Station pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Hivi karibuni tulipata fursa ya kufanya naye mahojiano ambapo tuliongelea mambo mengi kuhusiana na kazi yake ya utangazaji,maisha yake binafsi na mipango yake ya baadaye.Kumbukumbu na uwazi alionao Fina ni jambo ambalo limetuvutia sana. Unataka kujua Fina anasemaje kuhusu maendeleo ya kisayansi na kitekinolojia ulimwenguni? Asingekuwa mtangazaji angependa kuwa nani?Je umeshawahi kuona picha za utotoni za Fina? Fuatana nasi katika mahojiano haya ya pekee. read more

Hapo zamani kidogo studio za kurekodia nchini Tanzania zilikuwa ni chache sana kama sio hakuna kabisa. Studio ya Radio Tanzania Dar-es-salaam(RTD) ndio ilitumiwa na bendi zote au mtu yeyote aliyetaka kurekodi. Kama sio RTD basi ilikuwa ni kwenda Nairobi,Kenya kama unataka kurekodi.

 

Mambo siku hizi yamebadilika.Studio zipo kibao.Kinachotakiwa ni hela yako tu na kipaji. Kipaji ni muhimu kwani sio kila mtu amezaliwa kuwa mwanamuziki.Wengine tunaweza kubakia kuwa mashabiki na kisiharibike kitu. Mojawapo ya studio hizo ni Big Time Records ambayo inamilikiwa na produza Said Comorie (pichani)

Picha kwa hisani ya MichuziJR

↑ Go Back to Top of Page