MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Ijumaa imewadia.Kama kawaida hii ni siku ambayo watu wengi,hususani wanaofanya kazi ya Jumatatu hadi Ijumaa,huwa wanaisubiri kwa hamu. Hapo sijasema kwamba wikiendi hii ni “Mwisho wa Mwezi”.Kila mtu anazo.Bahati nzuri ni kwamba bado tupo katika Mwezi wa Toba kwa hiyo vibweka huko mitaani navyo huwa vinapungua. La sivyo,ungesikia vibweka kutoka katika baa ya kona.Sikia vicheko.Sikia jinsi baa medi anavyokaripiwa akichelewa kuweka bia mezani.Jeuri ipo.Pesa huwa inaongea.

Nasi hapa BC,tupo kwa ajili ya kuendeleza jadi.Ijumaa ni siku ya kujifaragua kidogo.Zamani walikuwa wanasema siku ya “kuruka majoka”.Ni wakati wa Zilipendwa. Leo tungependa kukuhamisha kidogo msomaji na mpenzi wa safu hii ya kila Ijumaa.Hatukupeleki mbali sana.Ni hapo DRC.Zamani iliitwa Zaire.Ilikuwa maarufu sana ulimwenguni hususani baada ya ule mpambano wa ndondi za uzito wa juu baina ya Mohamed Ali na George Foreman mwaka 1974. Enzi za Mobutu Seseseko Nkuku wa Zabanga.

Wimbo unaitwa Mamou(Tu Vois?) kutoka kwa gwiji la magwiji katika Afro-Rumba.Si mwingine bali mzee mzima Francois Luambo Makiadi maarufu kama Franco.Wimbo huu ni hadithi tamu sana.Hadithi ya mapenzi,uongo katika mapenzi,maisha nk. Zamani nakumbuka tulikuwa tukitaniana kwamba wimbo huu na mwingine hivi wa Madilu System,ulikuwa ukiuanza basi unasafiri kutoka Dar-es-salaam mpaka Morogoro na bado unaburudika tu.

Naamini wimbo huu unaweza kukukumbusha mbali.Usiwe mchoyo basi wa kuwaambia wenzako kupitia sehemu ya maoni kwamba Mamou inakukumbusha wapi.Ulikuwa unasakata Rhumba sehemu gani? Nakutakia wikiendi njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Ukitaka kusoma tafsiri ya Kiingereza ya wimbo huu bonyeza hapa.

JKN

JK

JKN

He was born on 4th August 1961,just few months before Tanganyika got her Independence. Today he turned 49! We join millions of people in the world to wish him a Happy Birthday.

He smiled when he was a young boy.

He is now the first African American president and yes…he is still smiling!

First Family ikielekea mapumzikoni hivi karibuni.Hivi sasa kuna mijadala kadhaa katika mitandao ya kijamii kama FaceBook,Twitter nk kuhusu muonekano wa Rais Barack Obama.Wengi wanasema kwa muda mfupi tu ambao amekuwa Rais,jamaa anaonekana kuzeeka kwa kasi.Ni kweli?

Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni,bado wanaendelea na uchunguzi wa kifo cha kushtusha cha Prof.Mwaikusa, mpwa wake,Gwamaka Daudi na jirani yake mfanyabiashara John Mtui.Hizi hapa ni picha kutoka nyumbani kwa marehemu na kutoka kwenye tukio hilo la kinyama.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam,Prof.Rwekaza Mukandara(aliyesimama kushoto) akiongea na waandishi wa habari kuhusu msiba huo mzito.

Baadhi ya waombolezaji waliofika nyumbani kwa marehemu.

Nyumbani kwa Marehemu Prof.Mwaikusa maeneo ya Salasala jijini Dar-es-salaam.Pembeni yake ni gari alimopigiwa risasi zilizosababisha kifo chake.Marehemu alikuwa akirejea nyumbani kwake kutoka katika shughuli zake majira ya saa nne usiku.

Kiatu cha Marehemu Prof.Mwaikusa kilichobaki katika eneo la tukio baada ya kuuawa.Katika mlango wa gari ni damu ya marehemu.

Polisi wakiendelea na uchunguzi katika eneo la tukio.

Polisi wakipata maelezo kutoka nyumbani kwa jirani mfanyabiashara,John Mtui, aliyeuawa wakati akienda kutoa msaada kwa marehemu Prof.Mwaikusa.

Picha zote kwa msaada wa Bashir Nkromo na Haki Ngowi.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Bila shaka uliona sherehe za ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA yanayoendelea nchini Afrika Kusini.Kama jibu ni ndio,bila shaka unakumbuka wimbo alioimba R.Kelly akishirikiana na Soweto Gospel Choir.Hii hapa ni Official video ya wimbo huo;Burudika

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Bila shaka umezipata habari ambazo zimeshaenea sehemu mbalimbali ulimwenguni kuhusu kukamatwa na kisha kuachiwa kwa dhamana(kajiwekea mwenyewe mdhamana)Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Joseph Mbilinyi aka Mr. II alias Sugu.

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo blogs ya Issa Michuzi na Da,Subi(wavuti dot com) sababu za kukamatwa kwake leo na maafisa wa jeshi la Polisi akiwa katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakati wa kikao cha kuongelea masuala ya muziki, ni kufuatia mmoja wa viongozi wa kituo kimoja  cha redio ya jijini Dar Es Salaam kumshitaki kuwa anamtishia maisha kwenye wimbo mmoja ambapo Mr. II anasikika akisema “I wanna kill you”. Wimbo huo na nyinginezo zinapatikana katika albamu ya ‘Anti-Virus’ inayosambazwa bure mtaani.

Katika utetezi wake,Mr. II ambaye alitarajiwa kutangaza nia yake ya kuwania Ubunge mkoani Mbeya kwa tiketi ya CHADEMA,anasema jambo hilo limemshangaza kwa kuwa maneno yaliyotumika katika wimbo huo ni ya kisanii zaidi na yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja.

Amedai alikamatwa na kuhojiwa na maofisa wa Polisi kutoka Makao Makuu ya jeshi hilo kwa saa kadhaa na kisha kuachiwa kwa dhamana ya kujidhamini mwenywe, na ametakiwa kuripoti kituoni hapo kesho kutwa.

Mr. II pamoja na wasanii wengine wamerekodi nyimbo kadhaa na kuweka kwenye albamu moja ambayo wameiita Anti-Virus, wakielezea hisia zao mbalimbali za kimaisha na kadhia la muziki wa Tanzania.

Je,hii na haki na sahihi(kwa Sugu kufikishwa katika mkono wa sheria)  au ni uonevu? Ni kweli kwamba inawezekana Sugu amekamatwa kutokana na juhudi zake mpya katika ulimwengu wa siasa ambapo hivi karibuni yeye na baadhi ya wasanii walitangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)?

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page