
Miss Universe Tanzania 2010,Hellen Dausen,will be onstage tonight to proudly represent Tanzania at the global Miss Universe 2010 beauty pageant.
TheMiss Universe 2010 which is the 59th edition of the pageant,will be held at the Mandalay Bay Events Center in the Mandalay Bay Resort and Casino,Las Vegas-Nevada,US. It will be hosted by Bret Michaels and Natalie Morales.It will be broadcasted Live on NBC starting at 9pm Eastern Standard Time.
Goodluck Hellen.
UPDATE: The Miss Universe Pageant is Live right now on NBC.That comes with a bit bad news;The top 15 contestants have just been announced and Hellen Dausen is not among them!That means,once again,we gonna have to wait and hope for next year.The only contestant from Africa who is in top 15 is Miss Universe-South Africa.
Top 10: Ireland,Albania,Philippines, Jamaica,Mexico,Ukraine,Puerto Rico,South Africa,Guatemala and Australia.
Miss Congeniality: Australia
Miss Photogenic: Thailand
National Costume Award Winner: Thailand
Top 5: Mexico,Jamaica,Ukraine ,Phillipines and Australia
4th Runner Up:Phillipines,
3rd Runner Up: Ukraine
2nd Runner Up: Australia
1st Runner Up: Jamaica
MEXICO WINS MISS UNIVERSE 2010!
Miss Universe 2010: Mexico

Josefina Nunez, Miss British Virgin Islands 2010; Qory Sandioriva, Miss Indonesia 2010; and Hellen Dausen, Miss Tanzania 2010, pose in their Dar Be Dar swimsuits during the registration and fitting process in preparation for the Miss Universe 2010 Competition at Mandalay Bay Hotel and Casino in Las Vegas, Nevada on Sunday, August 8, 2010. The Miss Universe 2010 competition that will air live on the NBC Television Network at 9 PM ET, August 23, 2010

Miongoni mwa mahojiano ambayo yamewahi kutia fora hapa BC ni pamoja na yale niliyowahi kuyafanya na Miss Tanzania 2007,Richa Adhia(pichani). Kama hukuwahi kuyasoma,unaweza kufanya hivyo sasa.
Sasa jana kuna msomaji mmoja kaniuliza;yuko wapi hivi sasa Richa? Kwa faida yake na ya wengine ambao wanaweza kuwa na swali hilo mioyoni mwao,jibu ni kwamba sina uhakika sana.Juhudi zangu za kutaka kufanya naye mahojiano mengine kuhusu anachotarajia kufanya baada ya kuvua taji la Miss Tanzania,ziligonga ukuta.
Ila kwa mujibu wa tovuti ya Miss Tanzania, Richa hivi sasa yupo jijini Dar-es-salaam akiwa amefungua clinic yake ya masuala ya urembo inayoitwa Beauty Clinic maeneo ya Mikocheni.Bado ana ndoto za kufungua chuo au shule ya masuala ya urembo.
Kesho ndio kesho. Mshindi lazima apatikane.Mwakilishi wetu katika mashindano ya ngazi ya dunia ya Miss Universe atajulikana hapo kesho tarehe 23/4/2010 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam. Jumla ya warembo 20 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania,wameteuliwa kuwania taji hilo ambalo bila shaka sote tunakubaliana kwamba ni miongoni mwa mataji ambayo mpaka sasa yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitangaza nchi yetu ya Tanzania na kuiletea sifa kimataifa.
Tukio la kesho litasindikizwa na burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii kama vile Nameless kutoka Kenya,Nakaaya, Mama Afrika Circus na wengineo kibao.
Hizi hapa ni picha za warembo wanaotarajiwa kushiriki hapo kesho.Photography by Moiz Hussein, Stylist and designer Farouque Abdela, Make up – Oriflame International. Unadhani mrembo yupi ataibuka mshindi?
Kama bado hujajipatia ticket yako, tafadhali piga simu 0784 305122 au nenda pale Shear Illusions shops ndani ya Millennium Towers na Mlimani City.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Tabia-anatokea Dodoma na aliyepo kulia anaitwa Selina kutokea Dar-es-salaam.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Sanje-anatokea Dodoma na aliyepo kulia anaitwa Rose kutokea Dodoma.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Redempta-anatokea Morogoro na aliyepo kulia anaitwa Neema kutokea Dar-es-salaam.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Nasra-anatokea Dar-es-salaam na aliyepo kulia anaitwa Mwajabu kutokea Mwanza.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Maureen-anatokea Morogoro na aliyepo kulia anaitwa Mary kutokea Morogoro.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Josephine-anatokea Dar-es-salaam na aliyepo kulia anaitwa Immaculata kutokea Mwanza.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Hellen-anatokea Arusha na aliyepo kulia anaitwa Halima kutokea Arusha.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Gaudencia-anatokea Morogoro na aliyepo kulia anaitwa Demitria kutokea Dar-es-salaam.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Fatma-anatokea Dar-es-salaam na aliyepo kulia anaitwa Esther kutokea Mwanza.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Devotha-anatokea Dar-es-salaam na aliyepo kulia anaitwa Anna kutokea Dar-es-salaam.

KESI ya kushambulia na kuharibu mali iliyokuwa inamkabili Miss Tanzania, Miriam Gerard, pamoja na rafiki yake imefutwa na wawili hao pamoja na mtu wanae shitakiana nae sasa watamalizana nje ya mahakama.
Kwa mujibu wa blog ya Father Kidevu, Uamuzi huo umefikiwa leo katika Mahakama ya Kinondoni ambako kesi hiyo ilifikishwa mwezi Februari.
Bila shaka habari hizi ni njema kwa Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Uncle Hashim Lundenga ambayo kimsingi ndio msimamizi mkuu wa shughuli za kijamii zinazofanywa na mrembo huyo mpaka hapo atakapoachia taji lake.Life goes on.

Binti au mrembo unayemuona pichani anaitwa Lilian Mduda(21). Huyu ndiye mwakilishi wetu katika fainali za shindano la kumsaka Kisura wa Afrika kupitia Mnet(Mnet Face of Africa) zinatarajiwa kufanyikia jijini Lagos nchini Nigeria tarehe 6 Februari/2010. Jumla ya warembo 10 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ndio waliofanikiwa kuingia katika fainali hizo na kwa maana hiyo ndio wataochuana.
Warembo wengine waliofanikiwa kufikia fainali wanatoka katika nchi za Angola,Ethiopia,Ghana,Kenya,Mozambique,Nigeria,South Africa,Zambia na Zimbabwe.
Lilian Mduda ambaye ni mwanfunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akisomea Biashara(B.Comm), amesema amejiandaa vyema kwa ajili ya shindano hilo na haoni mshiriki yeyote anayemtisha isipokuwa ni yeye mwenyewe anayeweza kujiwekea mazingira ya kushinda kwa kuzingatia yale yote atakayoelekezwa na kuyafanya kwa ufanisi ili aweze kufikia malengo yake katika fainali hizo.
Lilian anapenda kusoma novels zenye hadithi za kimapenzi na chakula akipendacho ni wali na maharage.Ndoto zake ni pamoja na kuweza kutembelea jiji la Paris siku moja.Pia anapenda mpira wa kikapu(basketball) na hupenda kusikiliza mziki na kujisomea.Kila la kheri Lilian.
Ukitaka kujua zaidi kuhusu Mnet Face of Africa na warembo wengine wanaoshiriki,bonyeza hapa.

Visura 12 wa M-Net wanaowania nafasi ya kuchuana kwenye fainali za kumtafuta kisura wa Africa(M-Net Face of Africa) zitakazofanyika katika jiji la Lagos, Nigeria, Februari 6, 2010.

Ijumaa hii katika ukumbi wa Mlimani City,ni kivumbi na jasho.Mrembo wa Afrika Mashariki atakuwa akitafutwa. Zawadi kuu ni Toyota Celica Sports kama inavyoonekana pichani juu na huku warembo wanaowania taji hilo wakiwa wamelizunguka.
Nani atalinyakua gari hilo?Hilo ndilo swali la msingi. Kwa picha zaidi za warembo hao,na habari zaidi kuhusu tukio hili,bonyeza hapa.
Warembo wanaoshiriki katika mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa 2009 wataanza kuwasili nchini wiki hii(au wameshaanza kuwasili) tayari kwa mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi wa 12 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Aidha, warembo watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo wanatarajiwa kutangazwa kesho kutwa baada ya kamati maalumu iliyopewa jukumu la kuratibu zoezi hilo kukamilisha kazi yake.
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na Nchi zinazoshiriki mashindano hayo kuchagua warembo wenye viwango vya hali ya juu ili kuziwakilisha katika mashindano ya mwaka huu
Miss East Africa 2009 itashirikisha warembo kutoka katika Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, na Mauritius ambazo zote zimeshathibitisha ushiriki wao.
Mashindano hayo makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya jijini Dar es salaam.
Miongoni mwa makampuni yanayodhamini mashindano hayo kwa mwaka huu ni pamoja na Kunduchi Beach Hotel & Resort, EATV, Kings & Queens Worldwide, CMC Automobiles Limited na AKO Catering Services Ltd.
Hizi hapa chini ni picha,majina na umri wa baadhi ya washiriki wa mashindano hayo.

Rebecca Getachew (23) Ethiopia,
Asli Osman Mahamud(20)-Somalia
Fatma Abdilahi (18)-Somalia

Dalysha Nirena Doorga (21)-Mauritius

Tabitha(20)-Kenya

Queen Belle Monique (23)-Burundi

Majuzi Tanzania ilipata mrembo mpya(Miss Tanzania 2009) ambaye ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia ya urembo(Miss World) yanayotarajiwa kufanyikia nchini Afrika Kusini tarehe 12 December 2009.
Mrembo wa mwaka huu,Miriam Gerald,pia ndiye mshindi wa Shindano la Miss Redd’s Photogenic (mrembo anayevutia zaidi au mwenye mvuto zaidi katika picha). Shindano hilo linaratibiwa na Blogu ya Jamii iliyo chini ya Muhidin Issa Michuzi.Hongera Bro.
Pichani ni Meneja wa Bia ya Redds Kabula Nshimo(kulia)akimkabidhi Vodacom Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald zawadi ya mfano wa hundi ya shs milioni moja baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Miss Redd’s Photogenic 2009 wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe, Dar es Salaam juzi.
Kwa picha zaidi za hafla hiyo,bonyeza hapa.

