Recent Articles
YANGA YAICHAPA SIMBA 2-0/ MASHABIKI BARANI AFRIKA WAFURAHIA MECHI KUPITIA SuperSport EAST 9

YANGA YAICHAPA SIMBA 2-0/ MASHABIKI BARANI AFRIKA WAFURAHIA MECHI KUPITIA SuperSport EAST 9

Yanga wakifurahia mojawapo ya magoli kutoka katika mechi hiyo. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry Blog Timu ya soka ya Yanga, jioni hii imewadhihirishia mashabiki wao ...

Read More

PERONI JAZZ SUNDAYS @ VELISA’s

PERONI JAZZ SUNDAYS @ VELISA's

Jumapili hii Mei 19 kuanzia saa Kumi na Moja jioni hadi Saa Mbili usiku karibu uburudike na muziki laini wa Jazz ukiletwa kwako na Wakwetu ...

Read More

EVE JUU YA ALBUM YAKE MPYA, BOYFRIEND WAKE MPYA, DMX NK

EVE JUU YA ALBUM YAKE MPYA, BOYFRIEND WAKE MPYA, DMX NK

Takribani miaka 11 imepita tangu Eve alipotoa album yake ya mwisho. Habari njema ni kwamba sasa amerejea tena katika ulingo. Album yake ambayo imeshatoka inaitwa ...

Read More

RAIS KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA LISHE

RAIS KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA LISHE

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mama Maria Nyerere, Naibu Waziri wa Afya Dr. Seif Rashid wakipozi na wakuu wa mikoa ...

Read More

“RIZIKI YANGU”- LINEX Feat.WYRE

RIZIKI YANGU- LINEX Feat.WYRE

Linex ft. Wyre - riziki yangu Hakuna ubishi kwamba Linex ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wenye kipaji cha hali ya juu katika uimbaji ...

Read More

KIBOKO CHANGU-AMANI Feat.RADIO & WEASEL (NEW VIDEO FROM OGOPA DEEJAYS)

Here is a latest one from Amani Feat. Radio & Weasel. The song title: KIBOKO CHANGU [youtube:https://www.youtube.com/watch?v=b9SzVjb0csc]

Read More

“NIPE NAFASI”-BARIDI -YOU CAN NOW OWN IT

NIPE NAFASI-BARIDI -YOU CAN NOW OWN IT

Wapo wasanii ambao bado hawana majina makubwa.Hawa wanahitaji support yako hususani kwa wale ambao wana kipaji.Mfano mzuri ni huyu.Anaitwa Baridi.Single yake ambayo aliitoa mwaka jana ...

Read More

BONDIA FLOYD MAYWEATHER JR.AONGOZA KWA KIPATO KIKUBWA KWA MWAKA WA PILI MFULULIZO

BONDIA FLOYD MAYWEATHER JR.AONGOZA KWA KIPATO KIKUBWA KWA MWAKA WA PILI MFULULIZO

Bondia Floyd Mayweather Jr, ndiye mwanamichezo mwenye kipato kikubwa zaidi miongoni mwa wanamichezo katika aina mbalimbali za michezo nchini Marekani au Marekani ya Kaskazini kwa ...

Read More

YANGA Vs SIMBA: SHUHUDIA MECHI HII “LIVE” KUPITIA SuperSport (DStv)

YANGA Vs SIMBA: SHUHUDIA MECHI HII LIVE KUPITIA SuperSport (DStv)

Upo msemo wa Kiswahili unaosema "Mafahali wawili wapiganapo,ziumiazo ni nyasi". Kama kuna ukweli wowote kwenye msemo huo, basi ni dhahiri kwamba wanapombana Yanga na Simba, ...

Read More

MSTAHIKI MEYA JERRY SLAA AFUNGUA TAWI JIPYA LA OFISI ZA DStv TANZANIA BARABARA YA MSIMBAZI KARIAKOO JIJINI DAR.

MSTAHIKI MEYA JERRY SLAA AFUNGUA TAWI JIPYA LA OFISI ZA DStv TANZANIA BARABARA YA MSIMBAZI KARIAKOO JIJINI DAR.

Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Furaha Samalu katika hatua za mwisho za maandalizi kabla ya kuwasili kwa ...

Read More

DIAMOND ON SPORAH SHOW: TOFAUTI NA UJUAVYO…

DIAMOND ON SPORAH SHOW: TOFAUTI NA UJUAVYO...

Sijui...lakini nadhani sijawahi kumsikia Diamond akiongelea mahusiano yake na wanawake mbalimbali ukiwemo uhusiano wake na  Wema Sepetu ambao mara kwa mara umekuwa lulu ya magazeti ...

Read More

BIG BROTHER AFRICA 8: THE CHASE…

BIG BROTHER AFRICA 8: THE CHASE...

Ndani ya wiki mbili zijazo wapenzi wa vipindi au matukio mbalimbali yanajojiri kwenye luninga barani Africa watakuwa na kila sababu ya kuwa “busy” Msimu mpya ...

Read More



Lisa Jensen,mrembo ambaye jina lake na sura yake sio ngeni miongoni mwa wengi,ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World 2012 yanayotarajiwa kufanyika tarehe 18 August huko Ordos,Inner Mongolia,China katika ukumbi wa Dongsheng Fitness Center Stadium. Mashindano ya dunia ya urembo mwaka huu ni mashindano ya 62 kufanyika.

 

 

Be Sociable, Share!

KUJUA ZAIDI KUHUSU KILICHOJIRI BONYEZA LINK HII

Be Sociable, Share!
Mrembo huyo ni  Miss Akuot Philip Suzan (20)  mwenye urefu wa futi 6.1 anaekaa Juba, Sudan  ni mwanamitindo nchini humo na anatarajia kujiunga na Chuo Kikuu Cha Makerere Nchini Uganda mwaka huu.
Warembo ambao tayari wameshapatikana kutoka katika Nchi mbalimbali kwa ajili ya mashindano hayo ni mwakilishi wa Eritrea: Miss Rahwa Afeworki (22), kutoka Ethiopia ni: Miss Lula Teklehaimanot (19) na Miss Ayisha Nagudi (23) ambae ni mwakilishi wa Uganda.
Nchi zilizobaki zinaendelea kutafuta wawakilishi watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa 2012 ambayo yatazishirikisha Nchi 16 za ukanda huu ambazo ni Tanzania (wenyeji), Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine ni Southern Sudan, Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia pamoja na visiwa vya Mauritius, Madagascar, Comoros, Reunion na Seychelles.
Mashindano ya Miss East Africa ndio mashindano makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Africa.
Fainali za mashindano ya Miss East Africa ambazo huandaliwa na kumilikiwa na Kampuni ya Rena Events Ltd, zitafanyika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam, Tanzania.
Be Sociable, Share!

Warembo watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu wanaendelea  kupatikana kutoka katika Nchi mbalimbali zinazoshiriki mashindano hayo.

 

Mrembo mwingine aliyeingia fainali ni Miss Lula Teklehaimanot (19) kutoka Nchini Ethiopia ambae alipatikana mwishoni mwa wiki baada  ya kuwashinda warembo wenzake waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Ethiopia katika fainali hizo.

 

Miss Lula Teklehaimanot ana urefu wa 1.79m  na uzito wa 52kg ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha St. Merry University cha jijini Addis Ababa, Ethiopia ampapo anasomea degree ya Marketing

 

Pia Mrembo huyo ni miongoni mwa wanamitindo maarufu  wanaochipukia kwa kasi Nchini Ethiopia.

 

Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.

 

Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam

Be Sociable, Share!

Huwa nikisikia kuna mtanzania anashindani mahali,hususani nje ya mipaka ya Tanzania,akiwa amebeba bendera ya nchi yetu kwa njia moja au nyingine,huwa nasisimka na kujiuliza nawezaje kumsaidia ili ashinde.Ni hulka ambayo imeshajijenga ndani yangu kwa sababu pengine naelewa zaidi umuhimu wa kuitangaza nchi yetu kupitia mashindano mbalimbali,rasmi na yasiyo rasmi.Sekta nyingi muhimu ikiwemo utalii,misaada,mahusiano ya kimataifa nk huchangiwa sana na kukuzwa kwa jina la nchi yetu.

Ndio maana nilipopata habari ambazo nitakwambia hivi punde,nimeona nikushirikishe nikiamini kwamba na wewe unapenda watanzania wenzako wafanye vizuri.Habari ni kwamba binti yetu,mtanzania mwenzetu,Precious John ambaye hivi sasa anashikilia taji la Miss United States International University(USIU) kwa mwaka 2011,yupo mashindanoni tena safari hii akiwania taji la Miss University Kenya kwa mwaka 2012. Yeye ni miongoni mwa washindani ambao wanapewa nafasi nzuri ya kushinda.

Ili ashinde,na kama ilivyo kawaida ya mashindano mengi siku hizi,upo ushiriki wa mtandaoni.Na hapo ndipo unapohusika.Kura zetu zitachangia kwa asilimia 60% za kura zote.Unaweza kupiga kura yako pale www.pambazuka.co.ke. Haya sasa twende tukawaonyeshe wapinzani wetu wa jadi(Kenya) kwamba tunaweza! Mwisho wa kupiga kura ni tarehe 20 January siku ambayo ndio kilele cha mashindano hayo.Unaruhusiwa kupiga kura kila baada ya masaa 12.

Precious

A peackcock like dress

 

 

Be Sociable, Share!

Pichani ni Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Israel,akipunga mkono wa kwaheri kwa baadhi ya ndugu,jamaa,marafiki na watanzania waliojitokeza kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere(JNIA) jijini Dar-es-salaam hapo jana.

Salha ameondoka kwenda kushiriki katika mashindano ya dunia (Miss World) yatakayofanyikia jijini London nchini Uingereza mwezi ujao tarehe 6 Novemba katika ukumbi wa Earls Court Two ambapo mshindi wa Miss World 2010,Mmarekani Alexandria Mills atakabidhi taji lake kwa mshindi mpya.

Swali kubwa ambalo najiuliza na ningependa nawe msomaji ujiulize ni kwamba je,mwaka huu Tanzania ina matumaini ya kufanya vizuri zaidi kuliko miaka ya nyuma?Tumefanya maandalizi ya kutosha ili kwenda kushindana na sio kushiriki katika mashindano haya?Na endapo tutaishia kuwa wasindikizaji,mwakani tujiandae namna gani?Tuwapate vipi wanaokwenda kutuwakilisha?

Bila shaka majibu ya baadhi ya maswali hayo magumu yapo mikononi mwa Kamati ya Miss Tanzania.Kwetu sisi hapa BC,tunamtakia Salha kila la kheri.

Be Sociable, Share!


Amaya ni Beauty Salon & Spa mpya na  ya kisasa kabisa iliyopo katikati ya Jiji la Dar-es-salaam.Ipo nyuma ya jengo la Air Tanzania Corporation(ATC) lililopo katika makutano ya barabara za Ohio Street  na Garden Avenue.Amaya Beauty Salon & Spa inajivunia kuwa Beauty Salon & Spa inayotumia bidhaa halisi(original) kutoka Canada na USA huku ikiwa na wafanyakazi waliobobea katika masuala yote yanayohusu urembo kutokea ndani mpaka nje na wenye ujuzi wa kimataifa.

Miongoni mwa huduma zinazopatikana ndani ya Amaya Beauty Salon & Spa ni pamoja na;

  • Huduma za nywele kwa aina zote za nywele kuanzia kunyoa au kukata style mbalimbali, kusuka,kuweka dawa,ku-steam, kuchana style mbalimbali,kushonea weaving aina zote,kubandika lace wigs,relaxing,kubandika kope,ku-bond nywele,kuweka aina zote za rangi kwenye nywele, kusokota dreads,kutinda nyusi kwa uzi,twisser na wembe, etc
  • Huduma maalumu(specialized treatments) kwa ajili ya mikono na miguu(Manicure and Pedicure) ikiwemo kuosha miguu kwa kutumia mask na paraffin, kuosha mikono,kupaka rangi,kubandika kucha aina zote za rangi mbalimbali/tips,acrylic powder na gel.
  • Tunafanya facial za aina tofauti tofauti  ikiwemo kutoa chunusi,madoa ya uso nk
  • Pia tunafanya waxing
  • Tunapamba maharusi,send off,kitchen party na special days kama vile graduation,ubatizo,kipaimara nk
  • Tunauza products mbalimbali kama vile Designers Perfumes kutoka kwa Usher,J-Lo,DKNY etc.Avon Products kama vile Powders,Colognes,body creams,shower gels nk.Make-Up products za Mac kama vile Studio Fix,Powders & Foundations,Eye Shadow,Lipsticks/gloss,perfumes nk
  • Pia tunatoa huduma zote zilizotajwa hapo juu katika vyumba maalumu(Private Rooms) na kwa kutumia products maalumu.

Baadhi ya wafanyakazi wa Amaya Beauty Salon & Spa

Amaya Beauty Salon & Spa inayo sehemu kubwa ya maegesho ya magari(Parking) yenye ulinzi wa uhakika.Ipo wazi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi(6am) mpaka saa moja jioni(7pm) Jumatatu mpaka Jumamosi.

Kwa mawasiliano zaidi tumia simu; 0716 604495, 0684 262924 na 0753 262 924

Be Sociable, Share!

Hatimaye zoezi lililochukua miezi kadhaa la kumtafuta mrembo mpya wa Tanzania kwa mwaka huu wa 2011(Miss Tanzania 2011),lilifikia kilele chake jana usiku katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam na mwanadada Salha Israel kuibuka mshindi na hivyo kuvikwa rasmi taji la Miss Tanzania 2011 kutoka kwa Genevive Emmanuel Mpangala(Miss Tanzania 2010) aliyekuwa akilishikilia taji hilo mpaka hapo jana.

Katika kilele cha shindano hilo lililodhaminiwa kwa kiasi kikubwa na kampuni ya Vodacom na kupambwa na burudani ya mziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wanaotamba Afrika Mashariki na Kati kama vile Diamond,Bob Junior,Kidumu na wengineo,mshindi wa pili alikuwa Tracy Sospeter na mshindi wa tatu akawa Alexia William.

Tunampongeza Salha kwa taji jipya.Lakini pongezi hizo ni vyema zikaenda na maswali magumu.Je,Salha anatoa matumaini kwa Tanzania kufanya Vizuri katika steji ya dunia(Miss World)?Je,Tanzania itaishia kuwa wasindikizaji tu katika fainali za dunia zinazotarajiwa kufanyika tarehe 6 November huko jijini London nchini Uingereza?Kuna lolote jipya ambalo Kamati Ya Miss Tanzania imejifunza kutokana na “uzoefu” wa miaka ya nyuma?

Upo ushauri ambao uliwahi kutolewa kwa kamati ya Miss Tanzania kupitia hapa BC.Je,umezingatiwa?Ni suala la kusubiri na kuona.

Miss Tanzania 2011,Salha Israel(katikati) akiwa na Tracy Sospeter(kulia-Mshindi wa Pili) na Alexia William(kushoto-Mshindi wa Tatu) mara baada ya kutangazwa mshindi.




Be Sociable, Share!

Ally Rehmtullah S/S 2012
Photography by:  Aliakber ‘aZh’ Zoeb
Location: The Moevenpick Hotel, Dar-es-Salaam
Hair & Make-UP: Rehema Sule
Models: Jewels, Neema, Salma, Anne, Nadia
Stylist: Joris Fernandes
Wardrobe managers: Titus Londo & Martin Kadinda

read more

Be Sociable, Share!

Mmoja kati ya warembo unaowaona hapo juu,tarehe 10 September mwaka huu ndani ya Mlimani City,atatwaa title mpya na atakuwa Miss Tanzania 2011.Jumla ya warembo 30 wameshaingia kambini tayari kwa mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa tena na Vodacom Tanzania.Je,nani atatwaa taji hilo?Je,mwaka huu Tanzania itang’ara katika stage ya kimataifa yaani Miss World?

Be Sociable, Share!

← Read the Previous PageRead the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page