MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

InaAfrika

Bendi maarufu kutoka Tanzania,InaAfrika Band,wapo ziarani katika nchi mbalimbali za bara la Ulaya wakiwa watumbuizaji rasmi wa onyesho maarufu linalojulikana kama Circus Der Sinne-Mother Africa. Kama hujawahi kuliona onyesho hili,tafadhali usikose hususani kama unaishi au unatarajia kutembelea bara Ulaya kuanzia mwezi December mpaka mwezi February.

Kwa ratiba kamili ya Circus Der Sinne-Mother Africa,bonyeza hapa. Heko kwa InaAfrika Band.Keep the star shining.

pindabc

Pichani ni Waziri Mkuu ambaye pia ndiye mgeni rasmi wa tamasha la siku tatu la utamaduni wa Mtanzania linalowakilishwa na jamii ya Washubi na Wahangaza kutoka wilaya ya Ngara Mkoani Kagera, akionyeshwa baadhi ya vyakula vya kiasili ya makabila hayo leo mchana ndani kijiji cha Makumbusho jijini Dar.

Tamasha hilo limezinduliwa rasmi leo mchana na Mh. Pinda ambalo litadumu kwa muda wa siku tatu kuanzia leo ndani ya kijiji cha Makumbusho,jijini Dar. Ukipata nafasi pitia mitaa ya makumbusho ukajionee utamaduni wa wahangaza na washubi.

frankbcNiliwahi kusikia mahali fulani watu wa nchi jirani na Tanzania wakisema kwamba Tanzania huwa inachelewa kidogo kuanza mambo lakini pindi wanapoanza huwa wanakuja juu kwa kasi ya ajabu! Bila kuingilia mazungumzo yao,jamaa wakawa wanataja mifano kama vile jinsi ambavyo Tanzania imepiga hatua kwenye shughuli za kisanii kama vile muziki na hivi sasa filamu.

Kuna ukweli ndani yake; tunaweza kuanza mwisho lakini tukawa vinara. Yote inategemea jinsi ambavyo tunaamua kujiweka na kusonga mbele. Mojawapo ni kukubali kwamba kuna kukosea na pia kujirekebisha. Hivi sasa sanaa ya filamu inazidi kukua nchini Tanzania. Inatia moyo sana kuona watu wa mataifa mengine wanaangalia filamu ambazo zinaitwa “za kibongo”. 

Pamoja na hayo kazi kubwa bado ipo mbeleni.Kama alivyowahi kusema Steven Kanumba tulipohojiana naye,kuna haja ya serikali kutoa support ya kutosha ili kuzidi kuinua sanaa hiyo. Marekani ipo hapo ilipo kwa sababu ilitangaza sanaa na sera zake za mambo ya nje kupitia kwenye filamu. Ikulu ya Marekani ina kitengo cha kushughulikia masuala ya filamu.Kama filamu itaonekana haijakaa “vizuri” kwa mujibu wa taratibu zao,basi haitoki.Mradi unakufa.

Lingine ni hili ambalo muigizaji Mohamed Mwikongi(pichani) almaarufu kama Frank katika uigizaji ameliongelea majuzi alipofanya mahojiano na jamaa wa Global Publishers. Frank anasema lazima wasanii na washika dau wote katika nyanja za filamu wakubali kukosolewa. Wazungu wanaita hii constructive criticism. Unapokubali kukosolewa unajipa nafasi ya ushindi kwani maana yake ni kwamba kesho utafanya kizuri zaidi.Lakini pia ipo haja ya wakosoaji kutokuwa “wabezaji”. Unapokosoa basi useme pia sababu zako na utoe ushauri wa kujenga kwamba nini kifanyike.Kwa mwendo huo filamu za kibongo zitazidi kupata jina na sio ajabu kabisa siku moja nasi tukaona Slumdog Millionare za kikwetu.

must

Sanaa ya ubunifu wa mitindo ya viwalo nchini Tanzania inazidi kukua.Leo hii sio jambo la ajabu kusikia habari za maonyesho ya mavazi.Pamoja na hayo, sanaa hiyo bado inahitaji kuongezwa nguvu kwa kuungwa mkono na wananchi na pia serikali. Tuipende mitindo ya kwetu na pia tununue mitindo na bidhaa za kwetu.

Miongoni mwa wabunifu ambao wanachangia kukua kwa sanaa hiyo ni kama wanavyoonekana pichani,Fatma Amour na Mustafa Hassanali.Hapo walikuwa pamoja wakati wa onyesho lililoandaliwa na Fatma na kuitwa Kakakuona.Onyesho lilifanyikia pale Dar Alive wiki iliyopita.

Photo/John Bukuku.

Kwa miaka nenda rudi,watu waishio katika miji ya pwani wamekuwa na jadi ya kutumia vyombo mbalimbali vya usafiri wa majini.Vyombo kama mitumbwi,ngalawa,ma-jahazi nk ndio vimekuwa mstari wa mbele katika kurahisisha shughuli za usafiri kwa watu waishio pwani na zaidi zaidi katika shughuli za uvuvi ambazo kwa wengi ndio chanzo chao kikuu cha mapato.

Lakini hivi karibuni vyombo hivyo vya usafiri vimeanza pia kuingia katika uwanja mpana wa burudani au michezo.Pameanzishwa vitu kama mashindano ya kukimbiza Ngalawa kama inavyoonekana pichani.Hapo ilikuwa ni huko Zanzibar hivi karibuni ambapo Issa Michuzi alishuhudia mbio za ngalawa(Canoe Race?).Hapo ngalawa na waendeshaji wake zilikuwa zinawekwa sawa tayari kwa shindano hilo ambalo lilishirikisha jumla ya ngalawa kumi na tisa(19)

Je unajua tofauti iliyopo kati ya Ngalawa,Mtumbwi na Jahazi?Tuelimishe.Hii ndio picha ya wiki.

Mwanahawa Ally(pichani) ni miongoni mwa waimbaji Taarabu maarufu nchini Tanzania. Mojawapo ya nyimbo zake ambazo zinajulikana sana ni kama ule wa Viumbe Wazito Part 1 na Part 2. Unaweza kutizama video za nyimbo hizo kwa kubonyeza hapa na hapa. Je Mwanahawa anapoimba kuhusu Viumbe Wazito anamaanisha nini haswa?

Mbali na kuwa na utajiri wa asili wa aina yake,Tanzania ni nchi ambayo inajivunia kuwa na wasomi maarufu ambao wametapakaa kote ulimwenguni wakifundisha katika mashule na vyuo mbalimbali au kuongoza vitengo nyeti katika idara za kimataifa na zenye uzito wa ki-dunia nzima.

Mmojawapo miongoni mwa wasomi hao ni Prof.Joseph Mbele(pichani),mtanzania anayefundisha katika Chuo cha St.Olaf kilichopo Northfield jimboni Minnesotta nchini Marekani.Miongoni mwa wasomi na wafuatiliaji wa mambo mbalimbali ya kitaaluma jina la Prof.Mbele sio geni hata kidogo.Prof.Mbele ni mtunzi wa kitabu maarufu sana kiitwacho Africans and Americans:Embracing The Cultural Differences.Kitabu hicho ndicho kinachotumika zaidi hivi leo mashuleni na katika taasisi mbalimbali(zikiwemo balozi mbalimbali) wanapokuwa wanawaandaa watu wao kuja kusoma, kutembea tu,kufanya kazi au tafiti mbalimbali barani Afrika.

Kutokana na kwamba kumekuwepo na mijadala mingi sana kuhusiana na masuala yote yahusuyo mila,tamaduni,desturi,maisha ya ughaibuni nk,BC tuliamua kumtafuta Prof.Mbele ambaye ni msomi anayetambulika kimataifa na mwenye mamlaka ya kutosha kuhusiana na maeneo yaliyotajwa hapo juu ili kupata maoni na mitizamo yake.Katika mahojiano haya,Prof.Mbele anafafanua mambo mengi sana kama vile’je kuna kitu kama mila,tamaduni na desturi za kitanzania?Kwanini watu wengi hivi leo hususani vijana wanazidi kubobea kwenye tamaduni za kimarekani?Kwanini aliandika kitabu hicho kilichotajwa hapo juu? Kama wanajamii tunakubaliana kwamba tumepoteza dira na muelekeo katika tamaduni,mila na desturi zetu,nini kifanyike?Kwa majibu ya maswali hayo na mengineyo mengi,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

 

Picha ya wiki hii ni ya huyo binti wa miaka kumi(10) anayeitwa Violet Sastoni kutoka kikundi cha burudani,sanaa na maonyesho kinachoitwa Splended cha jijini Dar-es-salaam.Violet alikuwa akifanya vitu hivi ndani ya kijiji cha Makumbusho jijini Dar juzi wakati wa wa tamasha lililoitwa Ya Kale Yanapokutana na ya Kisasa.Hii ndio picha ya wiki hii.Imepigwa na Ahmad Michuzi.

 

Mama Tecla Mjata(pichani)mmoja wa waigizaji wa filamu na michezo ya kuigiza wakongwe nchini Tanzania.Mama Tecla ni mmojawapo kati ya washiriki wa filamu ya Bongoland II kutoka Kibira Films International inayotarajiwa kutoka mwaka huu.Swali gumu ni kwamba,kama taifa,tunafanya nini kuwaenzi wasanii wetu wakongwe kama Mama Tecla Mjata?

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page