
Khadija Mwanamboka
Mwishoni mwa wiki iliyopita, kituo cha kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kilicho chini ya Tanzania Mitindo House(TMH), kilitimiza miaka mitatu(3) tangu kianzishwe.
Katika shamrashamra za kusheherekea miaka hiyo mitatu,BC ilipata nafasi ya kuongea na Bi.Khadija Mwanamboka,mbunifu maarufu wa mitindo nchini Tanzania ambaye pia ndio mwanzilishi wa kituo hicho ambacho kwa mujibu wa mahojiano niliyoyafanya naye miaka mitatu iliyopita,kuanzisha kituo kama hicho ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.
Ndani ya mahojiano haya,Khadija,anaongelea mambo mbalimbali hususani changamoto ambazo wamekabiliana nazo,mafanikio ambayo wameyapata tangu kuanzishwa kituo hicho na mipango yao ya baadaye.Fuatana nami katika mahojiano hayo;
BC: Bi.Khadija,kwanza kabisa nianze kwa kukupongeza wewe na watu wote wanaohusika na Tanzania Mitindo House(TMH) kwa kutimiza miaka mitatu. Je,ndani ya miaka mitatu iliyopita,mmekabiliana na changamoto zipi na unaweza kusema mpaka sasa mmepata mafanikio gani?
KM: Kwanza naomba nianze kwa kutoa shukrani,kwa niaba ya wenzangu wote tunaoshirikiana bega kwa bega katika kuendesha Tanzania Mitindo House.
Tukizungumzia mafanikio; Katika miaka mitatu iliyopita Tanzania Mitindo House imeweza kuboresha maisha ya watoto yatima ambao,kwa namna moja au nyingine, walishakata tamaa ya kuishi.Kutokana na kuwepo kwa kituo kama hiki, leo hii kila mmoja ana ndoto yake katika maisha.
Mafanikio mengine ambayo tumeyapata ni kwamba tumeweza kufikia lengo letu la kuwa na kiwanja cha kuchezea watoto yatima ili na wao wawe na uhuru wa kucheza na kufurahi kama watoto wengine walio na wazazi.
Pia tumeweza kutimiza lengo letu kuu la kusaidia jamii kwa kupitia mavazi au mitindo kwa kutangaza kazi zetu za ubunifu mikoani kama vile Dodoma ambapo tulifanya onyesho mwezi wa sita mwaka jana.Katika onyesho hilo,baadhi ya wabunge wetu walivaa mavazi yetu na kupita jukwaani kama wanamitindo. Pia tulifanikiwa kufanya onyesho la mavazi ambalo lilihudhuriwa na Rais wetu Jakaya kikwete kama mgeni rasmi kule Ngurdoto Arusha katika mkutano wa CPA. Vilevile kwa upande wa nje ya nchi, mwezi Octoba mwaka huu tulifanya maonyesho ya mavazi kule New Jersey na Washington DC nchini Marekani.
Changamoto kubwa inayotukabili ni ukosefu wa fedha ili kutimiza mipango mbalimbali tuliyonayo. Hapo ndipo tunapowaomba wahisani mbalimbali iwe ni mashirika ya umma au watu binafsi waendelee kujitokeza kutusaidia ili tutimize malengo mengi zaidi.
BC: Pamoja na juhudi za mashirika mbalimbali kama vile TMH katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ikiwemo watoto wasio na wazazi,wanaoishi mitaani nk,bado matatizo hayo yapo na yanaendelea kukua.Je,una wito gani kwa washika dau mbalimbali,serikali nk katika kusaidia sio tu watoto ambao tayari wanaishi katika mazingira magumu bali pia kusaidia kukua kwa tatizo hili? 

Alicia Keys,a Grammy Award Winner,is hiring. She is looking for a Superwoman to work with her as a blogger for her new site,new venture where she hopes to empower and connect women and help them find their inner “superwoman”.
The new website is, IAAS.com and it is named after one of her most popular song “I Am a Superwoman“. Alicia hopes that through internet she can bring women together to share dreams,goals,struggles and advice. Her dream is to create a neighborhood and an online community dedicated to women.
Are you a superwoman? Do you wanna work with Alicia Keys. Click here to apply.
Kila siku huwa napokea hoja,mapendekezo,ushauri kutoka kwenu wasomaji wa BC.Pia huwa napokea maswali mbalimbali.Nikiwa na ufahamu mkubwa juu ya swali lililoulizwa huwa najibu.Ninapokuwa sina jibu,wajibu wangu ni kutafuta jibu ama kwa kuomba msaada kutoka kwenu wasomaji na wachangiaji wa BC au vinginevyo. Leo nimepokea swali ambalo sina jibu kwani swali hili limeelekezwa moja kwa moja kwa celebrities. Mwenzetu mmoja ameuliza swali lililopo hapo chini na mwisho ametoa ombi.
Ningefurahi sana kama angalau celebrity mmoja angejitolea kulijibu. Sio lazima ajibu kama mwakilishi wa celebrities wengine,bali yeye kama mtu binafsi. Asante Allen kwa swali zuri.
Napenda kuwapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya. Nina swali dogo sana kwa hawa Bongo Celebrity kwamba mbona hatuwaoni wakiwa mstari wa mbele katika kuhakikisha nchi yetu inapunguza au kutokomeza kabisa vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
Mwezi wa kumi na mbili mwaka jana tulishuhudia mwana Mitindo mashuhuri nchini Uingereza Naomi Campbel akifanya onyesho la mitindo pale Movenpick kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na mtoto dunia nzima. Wanamuziki wetu, wanamichezo , wanamitindo na hawa wengine tunaowaita Bongo Celebrity wako wapi katika kuhakikisha nchi yao inafikia malengo ya milenia namba 4 na tano ifikao 2015.
Hongera kwa Stara Thomas kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha nchi yetu inapunguza vifo vya mama na mtoto kwa kiasi kikubwa. Napenda kuwakumbusha kuwa Tanzania bila vifo vya mama na mtoto inawezekana.
Timu ya taifa ilipocheza na Ivory Cost fedha nyingi sana zilipatikana.
Wachezaji hawa ni matokeo ya kina mama hawa ambao leo wanakufa kutokana na matatizo ya ujauzito. Tunaweza kutumia timu yetu ya taifa kupunguza pia vifo hivi vya mama na mtoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa viongozi wakubwa duniani wanaohakikisha nchi zao zinapunguza vifo vya mama na mtoto.
Nawaombatuungane pamoja kwa kutumia vipaji Mungu alivyotupatia kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa vipaji vyetu na umaarufu tulio nao katika jamii yetu.
Ukimuuliza mtanzania yeyote wa kawaida kuhusu tatizo kubwa linaloikabili nchi hivi sasa,jibu utakalopewa ni “ufisadi”. Hili ni tatizo ambalo mpaka hivi sasa linaelekea kuzidi tu kuota mizizi. Viongozi wetu nao wanawanyooshea wengine vidole. Wale wa chama tawala nao wananyoosheana vidole. Wanasema ndani ya chama chao kuna mafisadi wanne tu!Ni kina nani hao?Kama wanajulikana inakuwaje bado wapo?
Hivi ni nani atamfunga paka kengele? Tatizo tumeshalijua. Ni ufisadi. Ni kuporomoka kwa maadili ya ki-uongozi. Kujilimbikizia mali ndio ujanja kwa mujibu wa wale walio kwenye nafasi za kufanya hivyo. Uzalendo leo hii unaishia kwenye bendera na lugha tu. Ukiwaona wanavyokenua utadhani wanakujali. Kumbe wanajiuliza una shilingi ngapi mfukoni ili wazichukue.
Mama Maria Nyerere,mjane wa Baba wa Taifa, hivi majuzi ameuliza maswali ya msingi na kukemea kwa jinsi anavyoweza. Alikuwa huko Hai mkoani Kilimanjaro. Bonyeza hapa usome alichokisema na kuonya. Bidii hizi hazina budi kuungwa mkono. Isitoshe uchaguzi umekaribia.Huu ni wakati wa kusema Imetosha Sasa. Amka na mwamshe mwenzio.

Miongoni mwa wanawake ambao ni nyota,mfano wa kuigwa na ambao Tanzania inajivunia kuwa nao ni Prof.Anna Tibaijuka. Ni miongoni mwa wale wanawake ambao DaMija huwaitwa “Wanawake wa Shoka”.
Pamoja na hayo,hivi karibuni ulimwengu ulishuhudia cheo alichokuwa akikishikilia pale UN-Habitat yenye makao yake makuu jijini Nairobi-Kenya kikiota mbawa katika mazingira ambao wengi hawajaelewa wala kukubaliana nayo.Miongoni mwa wasiokubaliana na “kushushwa cheo’ kwa Prof.Tibaijuka ni wafanyakazi wenzake.
Je ni kwanini Ban Ki Moon amemshusha cheo mama Anna Tibaijuka wakati hata hivyo mkataba wake ulikuwa unaelekea ukingoni(2010)? Je kuna harufu ya ufisadi? Soma zaidi kwa kubonyeza hapa na kisha tizama taarifa ya habari hapo chini kisha uwe muamuzi.

Leo ni siku ya Wanawake Duniani(Women’s Day).Ni siku ambayo husheherekea mafanikio na mchango wa wanawake katika nyanja zote za maendeleo ya binadamu iwe ni kiuchumi,kijamii au kisiasa.Ni siku ambayo inatukumbusha sote umuhimu wa kipekee wa wanawake duniani.Hapa tunawazungumzia mama zetu,dada zetu,wake zetu,watoto wetu,shangazi zetu,binamu zetu,majirani zetu wanawake,marafiki zetu,maadui zetu nk.
Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani,James Brown, aliwahi kuimba “It’s A Man’s World but It Would Be Nothing Without a Woman”. Hilo halina ubishi.Dunia tuionayo leo kama dunia,inatokana na mchango mkubwa wa wanawake.Dunia si dunia bila mwanamke.Haipo.
BC inaungana na wote katika kusheherekea siku hii na pia kuwasihi wanawake,popote pale ulimwenguni, waendelee kufanya ambacho wamekuwa wakikifanya tangu mwanzo wa dunia hii.Happy Women’s Day.
Mtizame James Brown na Luciano Pavarotti hapo chini wakiimba Its A Man’s World.Mungu azilaze roho zao mahali pema.

Pichani ni Mheshimiwa Sofia Simba,ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM nchini Tanzania.
Mheshimiwa Simba alichaguliwa katika uchaguzi ambao unasemekana ulikuwa wenye upinzani mkali katika historia ya jumuiya hiyo.Alishindana vikali na Mh.Janeti Kahama.
Kama zilivyo chaguzi nyingi kinachofuata baada ya vuta nikuvute huwa ni kazi.Je unadhani ni matatizo gani ya msingi yanayowakabili wanawake wa Tanzania?Ungependa kumpa ushauri gani Mh.Sofia Simba kuhusiana na Jumuiya anayoiongoza?

Kwa wengi,nchini Tanzania na duniani,anabakia kuwa mrembo kutoka nchini Tanzania aliyeiwakilisha nchi yake katika shindano la dunia la Miss Universe mwaka 2007 na kuwa mshiriki wa kwanza aliyeamua kulipanda jukwaa akiwa kipara.Kwa wengine,wakiwemo ndugu,jamaa na marafiki zake,anabakia kuwa Flaviana Matata.
Hivi karibuni alilivua rasmi taji lake la Miss Universe Tanzania 2007 baada ya kulitumikia kwa muda wa mwaka mzima.Tulipata nafasi ya kuongea machache na Flaviana baada ya kumkabidhi rasmi mrembo mwingine,Amanda Sululu, taji la Miss Universe Tanzania. Hivi tunavyoongea tayari Amanda yupo nchini Vietnam tayari kabisa kwa shindano la Miss Universe litakalofikia kilele nchini humo tarehe 13 Julai mwaka huu.
Sasa kama sote tujuavyo,mwaka sio kitu kidogo.Mambo mengi hutokea,mengi huweza kusemwa nk.Je ni yapi aliyapitia ndani ya mwaka mmoja alipokuwa akishikilia taji la Miss Universe Tanzania 2007? Na si unakumbuka ule mkasa wa kuzimia siku ya kupima ukimwi?Nini hasa kilitokea?Ni kweli alikuwa anaogopa kupima afya yake?Ana mipango gani hivi sasa? Anampa ushauri gani Amanda na pia vijana wenzie? Kwa hayo na mengineyo mengi,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; 

Miongoni mwa wanawake wanaofahamika na kuheshimika katika fani ya sheria nchini Tanzania ni Jaji Eusebia Nicholas Munuo(pichani).Hivi leo yeye ndio Makamu wa Rais Mteule wa Chama Cha Majaji Wanawake Duniani(IAWT).Mbali ya cheo hicho,Jaji Munuo pia ndio Mwenyekiti wa Chama Cha Majaji Wanawake nchini Tanzania(TAWJA).Yeye ndio Hakimu wa kwanza mwanamke nchini Tanzania na pia Jaji wa kwanza mwanamke katika Mahakama ya Rufaa nchini Tanzania.
Miezi kadhaa iliyopita Jaji Munuo alifanya mahojiano maalumu na mwandishi Happy Katabazi kuhusiana na mambo mbalimbali ya kijamii,kisheria na pia kumhusu yeye binafsi.Je ni kweli kwamba Jaji huyu aliwahi kuamuru kwamba mumewe atiwe ndani kutokana na kuidharau mahakama?Ili kupata jibu la swali hilo na mengine mengi kumhusu Jaji Eusebia Munuo,bonyeza hapa uitembelee blog ya Happy Katabazi.
Photo/Happy Katabazi

Mbunifu wa Mitindo maarufu,Khadija Mwanamboka, akiwa pamoja na Shamim Zeze,mmiliki na mwendeshaji wa blog ya 8020 Fashions,hivi karibuni jijini Dar. Khadija Mwanamboka ni miongoni mwa waanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Tanzania Mitindo House ambalo linajaribu kusaidia watoto yatima na wasiojiweza nchini Tanzania. Mwaka jana tuliwahi kuongea kidogo na Mwanamboka kuhusiana na TMH.


sending...