Huwa nikisikia kuna mtanzania anashindani mahali,hususani nje ya mipaka ya Tanzania,akiwa amebeba bendera ya nchi yetu kwa njia moja au nyingine,huwa nasisimka na kujiuliza nawezaje kumsaidia ili ashinde.Ni hulka ambayo imeshajijenga ndani yangu kwa sababu pengine naelewa zaidi umuhimu wa kuitangaza nchi yetu kupitia mashindano mbalimbali,rasmi na yasiyo rasmi.Sekta nyingi muhimu ikiwemo utalii,misaada,mahusiano ya kimataifa nk huchangiwa sana na kukuzwa kwa jina la nchi yetu.
Ndio maana nilipopata habari ambazo nitakwambia hivi punde,nimeona nikushirikishe nikiamini kwamba na wewe unapenda watanzania wenzako wafanye vizuri.Habari ni kwamba binti yetu,mtanzania mwenzetu,Precious John ambaye hivi sasa anashikilia taji la Miss United States International University(USIU) kwa mwaka 2011,yupo mashindanoni tena safari hii akiwania taji la Miss University Kenya kwa mwaka 2012. Yeye ni miongoni mwa washindani ambao wanapewa nafasi nzuri ya kushinda.
Ili ashinde,na kama ilivyo kawaida ya mashindano mengi siku hizi,upo ushiriki wa mtandaoni.Na hapo ndipo unapohusika.Kura zetu zitachangia kwa asilimia 60% za kura zote.Unaweza kupiga kura yako pale www.pambazuka.co.ke. Haya sasa twende tukawaonyeshe wapinzani wetu wa jadi(Kenya) kwamba tunaweza! Mwisho wa kupiga kura ni tarehe 20 January siku ambayo ndio kilele cha mashindano hayo.Unaruhusiwa kupiga kura kila baada ya masaa 12.
Precious
A peackcock like dress

Two of Tanzania’s favorites,Professor Jay and Diamond will be performing in Milton Keynes tonite.Don’t miss this and check the flyer below for the upcoming shows from the same artists.Hakuna kulala mpaka kieleweke!
Bila shaka ushawahi kusikia jina la John Mahundi(pichani). Huyu ni miongoni mwa producers wakongwe kabisa wa muziki hususani wa kizazi kipya. Hivi sasa John Mahundi anaishi nchini Marekani ambapo pamoja na kuendelea na kazi zake zikiwemo za muziki,pia yeye ni kiongozi wa AACUSA (Muungano wa wasanii wa Afrika wanaoishi nchini Marekani)
Hivi majuzi mtangazaji Sunday Shomari wa Voice of America-VOA alifanya naye mahojiano kuhusiana na umoja huo .Haya hapa mahojiano kamili.Sikiliza.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Pichani ni Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Israel,akipunga mkono wa kwaheri kwa baadhi ya ndugu,jamaa,marafiki na watanzania waliojitokeza kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere(JNIA) jijini Dar-es-salaam hapo jana.
Salha ameondoka kwenda kushiriki katika mashindano ya dunia (Miss World) yatakayofanyikia jijini London nchini Uingereza mwezi ujao tarehe 6 Novemba katika ukumbi wa Earls Court Two ambapo mshindi wa Miss World 2010,Mmarekani Alexandria Mills atakabidhi taji lake kwa mshindi mpya.
Swali kubwa ambalo najiuliza na ningependa nawe msomaji ujiulize ni kwamba je,mwaka huu Tanzania ina matumaini ya kufanya vizuri zaidi kuliko miaka ya nyuma?Tumefanya maandalizi ya kutosha ili kwenda kushindana na sio kushiriki katika mashindano haya?Na endapo tutaishia kuwa wasindikizaji,mwakani tujiandae namna gani?Tuwapate vipi wanaokwenda kutuwakilisha?
Bila shaka majibu ya baadhi ya maswali hayo magumu yapo mikononi mwa Kamati ya Miss Tanzania.Kwetu sisi hapa BC,tunamtakia Salha kila la kheri.

Kwa Tanzania naweza kuwa sahihi nikisema kwamba “napenda kumtambulisha” kijana Chris Mhina,mtanzania anayefanya vizuri katika anga za muziki kutokea nchini Sweden kwani naamini sio watu wengi sana ambao wameshapata nafasi ya kumsikia Chris Mhina.Lakini kwa pande za kule Sweden,Chris Mhina hahitaji utambulisho sana kwani tayari ni miongoni mwa wanamuziki vijana wanaofanya vizuri sana katika za muziki.
Hivyo basi kwa heshima na taadhima,naomba nimtambulishe kwako wewe msomaji kijana huyu ambaye kwa mapana anapeperusha bendera ya Tanzania kupitia muziki huko Sweden na kote kwingineko hususani barani Ulaya.Ukitaka kujua mengi kumhusu Chris unaweza kufanya hivyo kwa kutembelea tovuti yake kwa kubonyeza hapa. Ili kupata kionjo kidogo tizama video hiyo hapo chini ya wimbo wake Last Dance.

Siku chache zijazo,studio inayomilikiwa na P-Funk aka Majani ya Bongo Records itakuwa inapaa katika anga za kimataifa pale itakapoachia kitu ambacho kimemshirikisha msanii maarufu kutoka nchini Marekani anayekwenda kwa jina la MIMS(pichani).
Kwa mujibu wa habari ambazo BC imezipata,msanii MIMS ambaye ana asili ya Jamaica na mkazi wa maeneo ya Washington Heights huko New York, atashirikiana na wasanii kadhaa wa Tanzania katika track hiyo.Orodha kamili ya wasanii ambao watashirikishwa katika kibao tarajiwa bado haijawekwa wazi lakini tetesi zinapasha kwamba watakuwa ni wasanii wakali kutoka Bongo.
Miongoni mwa nyimbo za MIMS ambazo ziliwahi kufanya vizuri sana katika chati za muziki ulimwenguni ni pamoja na ule wa This Is Why I am Hot.Unaweza kutizama video ya wimbo huo kwa kubonyeza hapa.
BC itakuletea mzigo kamili pindi utakapokuwa tayari!





sending...


