Mwandishi wa Habari za Burudani na Michezo wa Gazeti la Mwananchi ambaye pia ni Mtangazaji wa Times FM “Kituo cha Kazi” Henry Mdimu, mwishoni mwa wiki aliamua kuuaga ukapera baada ya kufunga pingu za maisha na Angel Peter.Tizama mambo yalivyokwenda katika tafrija ya shughuli hiyo kwa kubonyeza hapa kwenda kwa Brother Mroki
Kutoka kwetu hapa BC,;Kaka tunakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya wewe pamoja na mkeo.Stay blessed.
Two of Tanzania’s favorites,Professor Jay and Diamond will be performing in Milton Keynes tonite.Don’t miss this and check the flyer below for the upcoming shows from the same artists.Hakuna kulala mpaka kieleweke!

Pichani ni kundi la Orijino Komedi wakitoa burudani hivi karibuni wakati wa kampeni za kisiasa(bila shaka unajua ni kampeni za chama gani) huko Igunga,Tabora.
Ninapoona picha kama hizi kuna swali najiuliza;hivi kuna uhusiano wa aina gani kati ya siasa na vichekesho(Politics and Comedy)?Kama anavyopenda kusema rafiki yangu Mzee wa Changamoto,nami nawaza kwa sauti katika hili.

Msanii Christopher Brian Bridges au maarufu kama Ludacris kutoka nchini Marekani,anatarajiwa kutua jijini Dar-es-salaam mchana huu tayari kabisa kwa makamuzi ya kumalizia msimu wa matamasha ya Serengeti Fiesta kwa mwaka 2011.Ludacris ndiye anatarajiwa kuwa kivutio kikuu katika tamasha hilo ambalo litafanyikia Jumamosi hii ya tarehe 30 July katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar.Viingilio katika tamasha hilo vimepangwa kuwa elfu 15,000/Tshs kwa advanced tickets na 20,000/Tshs mlangoni.

Lipo jambo ambalo kimsingi,mapromota wanahitaji kulifahamu;kuheshimu mikataba. Kinyume cha hilo,matokeo yake ni aibu kama iliyojitokeza juzi jumamosi pale katika Hotel ya Golden Tulip ambapo mwanamuziki maarufu barani Afrika,Hugh Masekela kutoka Afrika Kusini alipogoma kupanda jukwaani kutokana na ukiukwaji wa sehemu muhimu ya mkataba.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Abdallah Singano,Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano cha Stanbic Bank ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa tukio hilo, Hugh Masekela aligoma kupanda jukwaani baada ya promota wa show hiyo,Heri Bomani kupitia kampuni yake ya Full Circle Africa Limited kushindwa kumlipa msanii huyo kitu ambacho bila shaka ni ukiukwaji wa kipengele muhimu cha mkataba!
Akiongea na waandishi wa habari jana katika hotel ya Southern Sun,Abdallah Singano amesema wao kama wadhamini wamesikitishwa sana na kitu kilichotokea na wanapanga kuwachukulia hatua za kisheria mwandaaji na kampuni yake.Pia amewataka wote ambao walikuwa wamenunua tiketi za onyesho hilo kumtafuta mwandaaji ili awarejeshee fedha zao.

The show that never was!
Kwa upande mwingine,Sauda Simba,alifanikiwa kutuliza japo kidogo roho za wapenzi wa muziki waliohudhuria kwa onyesho safi kitu ambacho kinazidi kumweka Sauda pazuri hususani miongoni mwa wapenzi wa Jazz.Good job Sauda!

Sauda Simba performing.Photo by Issa Michuzi
Jijini Dar siku hizi yupo mchekeshaji mmoja ambaye anazidi kujipatia mashabiki.Anaitwa Evans Bukuku na stand-up comedy yake hufanyikia pale Sweet Eazy(Oysterbay Hotel). Wiki hii BC ilipata nafasi ya kuhudhuria stand-up comedy hiyo.
Ingawa kuna mambo mengi ambayo yanahitaji marekebisho,(kama vile watu kulipa kiingilio na kushindwa hata kuingia mahali husika kwa sababu ya watu kufurika na sauti kuwa na mwangwi nk),naamini ni mwanzo mzuri na huenda siku moja tukawa na stand-up comedy kama zile za Kings of Comedy na Queens of Comedy kutoka US..au Def Jam kabisa.
Here are some images all taken by Ahmad Michuzi JR

Comedian Evans Bukuku

The audience: I am sure you can spot Muhidin Issa Michuzi,Jokate Mwegelo and Hasheem Thabeet, some of many celebrities in attendance.The event was hosted by Taji Liundi.

The audience…he sure can make people show their teeth!

The Miss Universe Tanzania beauty pageant has got a new queen. Her name is Nelly Kamwera. She was crowned the new Miss Universe Tanzania 2011 at the event held at Golden Tulip Hotel in Dar-es-salaam last evening. Click here for more photos from the event.


Mchezaji Netiboli Mwanaidi Hassan anayechezea timu ya JKT Mbweni,ameibuka mshindi wa tuzo ya jumla ya mwanamichezo bora nchini Tanzania kwa mwaka 2010 kupitia tuzo za Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania au TASWA(Tanzania Sports Writers Association) zilizotolewa usiku huu katika Hotel ya Movenpick jijini Dar-es-salaam chini ya udhamini wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited(SBL).
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Mwanaidi Hassan kushinda tuzo hiyo.Alishinda tena tuzo hiyo kwa mwaka 2009.Kwa ushindi huo,Mwanaidi alijinyakulia zawadi ya gari Toyota GX 100.
Pichani ni mgeni rasmi katika hafla hiyo,Makamu wa Rais wa Tanzania,Dr.Gharib Bilal,akimkabidhi Mwanaidi tuzo ya Mchezaji Bora Tanzania.Anayeshuhudia pembeni ni Waziri wa Vijana,Habari,Utamaduni na Michezo Dr.Emmanuel Nchimbi.
Photo:Ahmad Michuzi

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Benjamin William Mkapa,usiku huu amepewa Tuzo ya Heshima wakati wa tuzo za michezo zinazotolewa na Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini(TASWA) usiku huu katika viwanja vya Movenpick Hotel jijini Dar-es-salaam.Rais Mstaafu huyo amepewa Tuzo hiyo ya Heshima kutokana na mchango wake katika michezo nchini Tanzania hususani kwa mchango wake katika ujenzi wa uwanja mpya wa taifa ambao kwa namna ya kipekee umeiletea heshima mpya nchi ya Tanzania katika medani ya michezo ulimwenguni.
Akipokea tuzo hiyo,Mkapa alikiri kwamba katika kipindi chake cha kwanza cha urais,hakuwahi kuhudhuria hata tukio moja la michezo.Alikuwa na sababu.Priority zingine zilimkabili.Masuala ya uchumi.
Rais Mkapa alitumia fursa hiyo kukanusha habari “nyepesi nyepesi” kwamba uwanja ule ulijengwa kwa msaada wa Uchina kwa asilimia mia moja.Badala yake,Mkapa amesema,ukweli ni kwamba uwanja mpya wa taifa,ulijengwa kwa mgawanyo sawa wa gharama katika ya China na Tanzania.Kwa maana hiyo,China ilitoa asilimia 50 na Tanzania ikatoa aslimia 50.
Photo Courtesy:Othman Michuzi


sending...

