Recent Articles
Watch: “Nasema Nawe”-Diamond Platinumz Feat Khadija Kopa

Watch: Nasema Nawe-Diamond Platinumz Feat Khadija Kopa

One challenge that every artist faces day in and day out is to remain an artist. To circumvent that trap, creativity must be at high ...

Read More

“Nobody But Me(NBM)”-Vanessa Mdee Feat. KO

Nobody But Me(NBM)-Vanessa Mdee Feat. KO

Here is one thing I probably have never said before. When I heard that Vanessa Mdee was taking a leap of faith to jump from ...

Read More

Zitto Zuberi Kabwe

The Rise And...Of Zitto Kabwe

Before entering into the world of politics, the best advice anyone can get is to be clear on his goals and ambitions. That means you ...

Read More

“Leo Leo”-Jokate Featuring Ice Prince [Listen And Download]

Leo Leo-Jokate Featuring Ice Prince [Listen And Download]

If at times you fail to understand or follow what exactly does Jokate do, you probably not alone. She is one of those multi-talented people ...

Read More

The Photo That Will Always Haunt Afande Sele

The Photo That Will Always Haunt Afande Sele

When Afande Sele went on stage on this particular day, he probably didn’t have much to loose. All he wanted was to entertain and rock ...

Read More

What Professor Jay Has To Say About His Political Ambitions

What Professor Jay Has To Say About His Political Ambitions

You probably know by now that Professor Jay has set his target into becoming another artist turned into a politician and a Member of the ...

Read More

Youth: Don’t Just March. Ask Serious Questions And Demand Serious Answers!

Youth: Don’t Just March. Ask Serious Questions And Demand Serious Answers!

Sometimes politics can be above rocket-science. You need to eat, remain seated in order to properly understand it. You need to know very well how ...

Read More

Image Credit:www.tintup.com

How To Get Your Post Shared 1000 Times

Ask any seasoned blogger or online content developer you know about his/her innermost desire after putting together a post and hit “publish” button. His/her answer ...

Read More

“Nitalala Uzeeni”-DJ Choka Feat. Young Lunya, Country Boy, Deddy, Climax Bibo & Bgway

Nitalala Uzeeni-DJ Choka Feat. Young Lunya, Country Boy, Deddy, Climax Bibo & Bgway

DJ Choka is a DJ than an artist. However, art is something inside every mind that excels or can excel in anything that requires creativity. ...

Read More

The First First Lady-Mama Maria Nyerere-Alive And Kicking!

The First First Lady-Mama Maria Nyerere-Alive And Kicking!

She was the victim of a death-hoax this week. Rumors spread like a wildfire that she has passed away. It was untrue. She isn’t even ...

Read More

#ThrowBackThursday On BC: “MamaLand”-Yvonne ChakaChaka

#ThrowBackThursday On BC: MamaLand-Yvonne ChakaChaka

Among the “ladies” of African Music, I think it’s fair to say that Yvonne Chakachaka belongs to the top list. We could argue whether she ...

Read More

“Salima”-Linex Feat. Diamond Platinumz [Listen |Download|Watch Video]

Salima-Linex Feat. Diamond Platinumz [Listen |Download|Watch Video]

Here is a story of two talented artists; Linex and Diamond. Their lives’ crossroads meets when one goes to school with a beautiful young lady. ...

Read More

Pharrell Williams Na Robin Thicke Walifanya “Uhuni” Katika Wimbo Wa Blurred Lines. Waagizwa Kulipa Million$7.3

Pharrell Williams Na Robin Thicke Walifanya Uhuni Katika Wimbo Wa Blurred Lines. Waagizwa Kulipa Million$7.3

Katika zama tunazoishi hususani za tekinolojia inayokua kwa kasi namna hii, masuala ya haki miliki yanaendelea kuwa changamoto ya kidunia. Mfano ni uamuzi wa mahakama ...

Read More

Yanga na Simba Zaungana Katika Kampeni Ya “Imetosha”

Yanga na Simba Zaungana Katika Kampeni Ya Imetosha

Na Henry Mdimu Tangu asubuhi leo nilikuwa busy na awareness za uwanja wa Taifa katika mechi ya watani wa Jadi Yanga na Simba (picha ya pili). ...

Read More

#ThrowBackThursday On BC: “Come Into My Life”-Joyce Sims

#ThrowBackThursday On BC: Come Into My Life-Joyce Sims

If I could, I’d love to ask you all the details how your week went etc. That would all be immaterial. The weekend is around ...

Read MoreMbaraka+Mwinshehe

Unajua kama kuna kitu kinanifurahisha ninapoketi na kuanza kuchambua makbrasha ya muziki wa zilipendwa kwa ajili ya hii segment ya Ijumaa ya Zilipendwa ni kwamba huwa napata pia nafasi ya kusikiliza sio tu jinsi ambavyo wanamuziki wa enzi zile walijaaliwa ujuzi wa utungaji na pia mpangilio wa “muziki” mzima, bali pia huwa napata nafasi ya kuwaza mambo kadha wa kadha kwa mkupuo.

Kabla ya kuamua wimbo gani uende hewani ni lazima niangalie mazingira ya wiki nzima. Nasikiliza yangu ya moyoni na pia kusikiliza yale yanayojiri au yaliyojiri kwenye jamii. Nasoma na kuuliza. Ni kazi nzuri. Naipenda kwani licha ya kunisaidia kuondoa stress binafsi ninapozisikia nyimbo ambazo leo tunaziita Zilipendwa  nakumbuka mbaaali. Enzi zile sikuijua shida. Kila kitu kilikuwa sawa…unataka kujua kwanini? Nipigie simu tuongee.

Wimbo wa leo unaitwa Kigeugeu. Ni kutoka kwao Super Volcano.  Mbaraka Mwinshehe aliimba na Stephen Hiza mwaka 76 katika mtindo wa Masika! Enzi hizo naweza kusema ni tofauti na sasa. Enzi zile wanaume ndio walikuwa “vigeugeu”. Mtu alikuwa anaweza kuchumbia na bado akaingia mitini. La Haula leo…vigeugeu ni wengi.Wanaume kwa wanawake. Wa mjini tunasema Ngoma Droo. Lakini mwisho wa siku, mmoja lazima ashindwe.

Usikilize hapa chini. Wimbo huu uende kwake rafiki yangu Fidelis Tungaraza akiwa kule Ufini na waungwana wote wa kundi la ENZI ZETU ndani ya Facebook

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Be Sociable, Share!

img431a

Sina muda mwingi sana leo wa kuandika kile ninachokiwaza kichwani mwangu.Lakini kama ujuavyo, leo ni Ijumaa na sio mbaya tukakumbuka enzi zile za dansi.

Huu hapa ni wimbo Naomi kutoka kwao DDC Mlimani Park Orchestra (Nginde)

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Be Sociable, Share!

DDC

Nianze kwa kukuomba msamaha wewe mpenzi wa segment hii ya Zilipendwa hapa BC. Kwa majuma kadhaa nimeshindwa kukupatia “raha”. Yapo mambo yalikuwa yanajiri ambayo kimsingi yalisababisha nami niingie kwenye ule mkumbo wa “sababu zilizo nje ya uwezo wangu”.Nisamehe na tuendelee.

 

Wakati nikikagua maktaba yangu ya miziki “Zilipendwa”, neno “mtumwa” lilikatiza. Ajabu ni kwamba katika siku za usoni nimekuwa nikiwaza sana jinsi binadamu anavyoweza kurubuniwa mpaka kuwa “mtumwa” wa kitu fulani.Unaweza kuwa mtumwa, kwa mfano, wa mtu fulani kwa sababu ana kipato fulani au pesa.Atakachokisema basi unakimbia kama “zuzu” hivi kwa sababu tu anazo hela kukushinda. Huthubutu kumwambia hapana. Hubishi kitu. Unabakia kukenua tu meno na kujichekeshachekesha. Umekuwa mtumwa.

 

Hapa DDC Mlimani Park(Sikinde) wanayo pia maudhui kama hayo hapo juu. Watu(hususani wanawake) kukubali kuwa “watumwa” kwa watu fulani fulani kisa….pesa au kipato. Upo wapi utu wako? Upo wapi uhuru wako wa kutafuta chako? Upo wapi uwezo aliokupa Mwenyezi Mungu wa kutumia akili yako na hivyo kubakia huru japo kimtizamo na kimawazo?Zipo aina nyingi za utumwa. Ukiwa na muda unaweza kuziongeza.

 

Wasikilize DDC Mlimani Park na wimbo Sitokubali Kuwa Mtumwa. Uwe na weekend njema na kumbuka ukipiga masanga basi usikae kwenye kiti cha dereva. Nataka ufike salama ili kesho nyumbani kwako pasiwe na majamvi au mikeka.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Be Sociable, Share!

Mtu ni afya. Mtu ni chakula anachokula. Bila shaka umewahi kusikia misemo hiyo ambayo imethibitishwa kuwa kweli kwa miaka nenda, miaka rudi. Na siku hizi suala la afya limekuwa muhimu zaidi.Vyakula tunavyokula havina tena rutuba na vitamins zinazotakiwa. Tunaviita vyakula vya kwenye makopo. Yote hayo ni kutokana na ujanja au ujinga wetu wanadamu.Tumeharibu wenyewe ardhi tuliyopewa. Maendeleo yana madhara yake.

Mbaya zaidi, watu wengi hatujui tule vyakula gani. Elimu kuhusu afya inayotokana na vyakula sio maarufu ingawa umuhimu wake hauelezeki. Haishangazi basi kuona kwamba nyimbo kama hii inayotupambia Ijumaa ya Zilipendwa leo, inazungumzia suala la afya bora. Ni kutoka kwa Mbaraka Mwinshehe na Moro Jazz. Wimbo unaitwa Mama Chakula Bora.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Be Sociable, Share!

Mwisho wa wiki ndio umeshawadia. Jijini Dar-es-salaam, mitandao ipo bize.Ukimpigia mtu utakutana na ujumbe kwamba ‘mtumiaji unayempigia anaongea na simu nyingine”. Ni wakati wa kupanga miadi ya kukutana na marafiki,ndugu na jamaa.Wikiendi.

Sisi Ijumaa haiwi Ijumaa bila kuendeleza Jadi ya Zilipendwa.Leo tunao Kilwa Jazz mojawapo ya bendi ambazo zimewahi kutamba nchini Tanzania enzi hizo ambapo wenyewe  wanasema “music was music”. Nacheka Cheka ndio jina la wimbo. Wasikilize hapa chini…Weekend Njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Photo Credit: www.waterbucksafaris.com

Be Sociable, Share!

Kwanza ilikuwa juhudi za kila namna za kujiandaa na sikukuu ya Christmas. Tofauti na enzi zile ambapo Sikukuu kama Christmas ilimaanisha kukumbuka zaidi kuzaliwa kwa Yesu Kristo,siku hizi imekuwa zaidi kuhusu zawadi,kunywa nk.Ni biashara.Kuna siku maalumu kabisa.Wa magharibi wanaiita Boxing Day. Ilipopita hiyo maandalizi ya kuupokea mwaka mpya 2013 yakaanza.Maandalizi hayo huwa na maazimio kibao.Kuna wanaotaka kupunguza unene,kuna wanaotaka kuacha kuvuta sigara.Kuna wanaodhamiria kuweka akiba zaidi katika Benki nk.Malengo na maazimio.

Mwaka mpya ukawadia.Tukakumbatiana kwa furaha.Mwenyezi ametuwezesha kuuona mwaka 2013.Ni jambo la kushukuru na ikiwezekana kumpa Mungu sadaka iliyo njema.Ghafla mwaka ndio ushaanza kukata mbuga.Tayari weekend ya kwanza ya mwaka 2013 ndio hii hapa.

Jambo moja jema hapa BC ni kwamba tunapanga kuendeleza ile jadi ya kuburudika kila weekend na Zilipendwa.Tunaanza na wimbo Weekend kutoka kwa gwiji, marehemu Patrick Balisidya na Afro 70.Burudika,weekend Njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Be Sociable, Share!

Zimebaki siku chache sana kabla hatujasikia ving’ora vya bandarini, taa za angani zikiwaka,shangwe,vifijo na nderemo za kuukamilisha au kuumaliza mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013.Mwaka mpya huwa ni siku ya furaha. Ni siku ya kutakiana kheri kwa mwaka mpya na pia kwa wale ambao ni mabingwa wa kujiwekea malengo, huwa ni siku nzuri ya tathmini na mipango.Wanasiasa huwa wanapenda sana kuitumia siku hii kutoa “ahadi” mpya!Ni hulka na hatuna budi kuikubali.Ahadi.

Kama nilivyosema,bado siku chache. Ya Mungu pia huwa ni mengi kwa hiyo ukianza kufanya tathmini hivi sasa hutakuwa umekosea sana. The earlier, the better…wenzetu kwa lugha yao wanasema hivyo.Leo ni Ijumaa ya mwisho kabisa kwa mwaka 2012. Nilipotizama kalenda na kutambua kwamba hii ndio Ijumaa ya mwisho, nilipata wakati mgumu kidogo kuchagua kitu cha kuweka kwa ajili ya Zilipendwa. Hata kama ni Ijumaa na kuna sehemu za dunia ambapo theluji imemwagika kupita kiasi wakati kwingine kuna jua na joto lisilo la kawaida, jadi lazima iendelezwe. Katika waza na wazua,nikamkumbuka Mwanamuziki maarufu,Ndala Kasheba.

Miongoni mwa nyimbo ambazo Kasheba anakumbukwa nazo sana ni pamoja na Yellow Card. Ni mara ngapi(hata ndani ya mwaka 2012 tu) umesikia au wewe mwenyewe umesingiziwa jambo? Mara ngapi umesikia fulani kafariki, au fulani kafilisika? Pale kwenye kijiwe cha supu ya utumbo umeshasikia mangapi? Naam, Yellow Card ulikuwa ni ujumbe mkali baada ya yeye(Ndala Kasheba) kuwa amesingiziwa mambo kibao.Waweza kuusikiliza na kuona je wafanana na maisha yako au ya rafiki yako?

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Be Sociable, Share!

Kwa mapana na marefu hii imekuwa wiki ngumu sana kwangu. Kuona ya kwamba ningali nadunda na nipo hapa nimeketi na kuanza kuandika hiki ninachoandika, ni ushuhuda tosha kwamba Mwenyezi Mungu bado yungali ana madhumuni na maisha yangu! Ni jambo linalotia faraja.

Wakati nawaza na kujaribu kuchagua wimbo wa kuweka katika segment hii ya kila Ijumaa ya Zilipendwa, nilijishtukia nakumbuka baadhi ya mikoa na bendi kutoka katika mikoa hiyo ambayo niliwahi kutembelea na kuishi. Mojawapo ya mikoa hiyo ni Mkoa wa Tabora ambako mpaka leo bado nina ndugu wengi tu. Nakumbuka babu mmoja aliyekuwa akituuzia “mantalali”. Naikumbuka mitaa ya Isevya, Chuo Cha Uhazili Tabora(Mama zangu wadogo wamesoma pale). Nakatiza toka mjini na kupitia shule ya Sekondari Uyui. Pale nawacheki wajomba wanaosoma pale. Nakatiza mitaa,pembezoni kuna miti ya miembe, jua la mchana limeshakolea.Joto linalotoka kwenye mchanga sio kawaida. Nalihisi vilivyo ingawa nimevaa raba zangu kutoka “Bora” ambazo Babu alinipa kama zawadi ya Christmas…

Nilipowaza Tabora ndipo nikaanza kutafuta wimbo kutoka kwa Tabora Jazz ambayo ni miongoni mwa bendi zilizowahi kutamba vilivyo enzi zile. Nikausikiliza wimbo Dada Lemi(Lemmy)….huu hapa.Na wewe usikilize na uwe na weekend njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Picha kwa hisani ya Kijiwe Cha Kitime

Be Sociable, Share!

Wiki iliyopita tulikumbushana kidogo kuhusu mila na desturi kwa upande wa maandalizi ya ndoa kwa kuanzia kwenye suala la kupeleka Barua ya Posa ukweni. Shukrani sana kwa wote ambao mmeniandikia na wale mliochangia aidha kupitia hapa hapa au kupitia mitandao jamii(facebook.com/bongocelebrity na Twitter @bongocelebrity. Inatia moyo kuona kwamba upo mtu kama wewe ambaye bado unajali na kuamini kwamba njia zetu(katika mila na desturi nyingi) bado ni sahihi na zinapendeza kuzifuata japokuwa zinakabiliwa na upinzani mkali wa dunia kuwa kama kijiji.

 

Waliotusaidia na kumbukumbu ya wikiendi iliyopita walikuwa ni Moro Jazz chini ya uongozi wa Mbaraka Mwaruka Mwinshehe. Wimbo ulikuwa Mshenga Namba 1.Leo tunaendelea na Mshenga Namba 2.

 

Pata picha umejikusanya wataka kuchukua “jiko”.Unamtafuta jamaa ambaye unamuamini na kumkabidhi jukumu la kuwa mshenga. Unampatia fedha azipeleke ukweni ili ukamilishe mchakato. Baada ya hapo, huku ukiwa na imani kwamba kila kitu kinaendelea vizuri, unaanza kupokea barua kutoka ukweni. Unaulizwa “We bwana vipi?”…”kama umeshindwa,sema ili mtu mwingine achukue jiko”. Kichwa kinaanza kukuuma.Umezikwa. Mshenga kakuingiza mjini…

 

Mbaraka anauliza imekuwaje? Lakini anawaambia “ukweni” msijali,nivumilieni.Nitakuja mwenyewe kumaliza mambo. Burudika…Ijumaa njema

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Be Sociable, Share!

Mbaraka Mwinshehe na mkewe, Amney Shadad, siku ya ndoa yao tarehe 17/3/1972 mjini Morogoro.Unajua nani alitumwa kama Mshenga?

Juzi rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kuniuliza “Jeff, unajua jinsi ya kuandika Barua ya Posa?”. Lilikuwa swali la ghafla na hivyo ili kupata muda wa kutafakari kidogo, nami nikarudishia kwa swali “Kwanini, wewe barua ya posa ya nini?”.Akaniambia “swahiba wangu fulani anataka kuoa na hivyo tunahitaji kupeleka barua ya posa kwa wazazi wake”. Nikawa mpole. Ukweli ni kwamba sijawahi kuandika Barua ya Posa. Nimeshawahi kuandika barua za kila aina lakini sio ya Posa. Lakini kwa kuelewa kwamba rafiki yangu ameniuliza kwa sababu anajua mimi ni mwandishi na napenda changamoto za uandishi, nikamwambia basi atulie tu na kabla jua halijazama, atapata Barua ya Posa ambayo yeye na mwenzie wataipeleka na kisha kukaa wakisubiri majibu kwa hamu ya ndio au hapana. Ukiaminiwa na jambo fulani kuna sababu na hivyo kama linawezekana,basi lifanye.Urafiki ni kitu muhimu na adimu.

Nilichokifanya baada ya kukata simu ya rafiki yangu ni kuwasiliana na baadhi ya marafiki zangu wengine ambao najua kwa kiasi fulani bado wangali wakizingatia mila na desturi ingawa ukweli ni kwamba katika zama hizi za kukutana na kuachania katika Facebook kabla hata ya kuonana ana kwa ana, inakuwa ngumu kidogo kudumisha mila na desturi. Ni dunia ambayo endapo mababu zetu waliotangulia mbele za haki wanatuona tukihangaika nayo, basi wanajionea maajabu tu. Ni tofauti sana na ile waliyoishi wao.

Bahati nzuri, Babu yangu aliwahi kunisimulia mambo mengi sana kuhusu mila na desturi zikiwemo za masuala haya ya ndoa,posa,mahari nk. Aliwahi kunisimulia vizuri hata visa vya wakati yeye akitafuta mchumba. Yupo mmoja aliacha kumuoa kwa sababu tu, alipokuwa akienda kumtembelea, binti huyo alimsindikiza mpaka mbali sana kitu ambacho kiliashiria kwamba “huyo binti hajatulia”. Kwanini anaenda umbali mrefu vile kutoka kwao?!Wazee wetu walikuwa na mbinu kali sana za kujua Mr.Right na Ms.Wrong.Tumezikacha na kuziona hazina maana. Lakini tunachokishuhudia leo katika ndoa, ni ishara tosha kwamba pengine wao walikuwa sahihi na sisi tupo nje kabisa ya mstari. Babu na Bibi yangu hivi sasa wana miaka zaidi ya 60 katika ndoa!

Bahati nzuri rafiki yangu wa kwanza tu kumpigia, naye alikuwa na kumbukumbu nzuri tu kuhusu masuala hayo(Asante sana E.M).Nami nikamwambia ninachokumbuka kisha tukakubaliana kile ambacho kimsingi ni cha muhimu kuwepo kwenye Barua ya Posa.Nikaandika na kuweka sawa na kweli kabla jua halijazama, ikawa tayari na rafiki yangu akafurahi sana. Shangwe na vigelegele vipo njiani.

Nilipokuwa nikiandika, niliamua pia kupitia baadhi ya vitabu vya mila na desturi ambavyo ninavyo katika maktaba yangu. Napenda kusoma na nina vitabu vingi tu.Endapo wanangu watakua na kupenda kujisomea(Namshukuru sana Mama yangu kwa kunibidisha katika kujisomea) basi wanao urithi mzuri wa vitabu,majarida na magazeti. Nilipokuwa napitia vitabu mbalimbali nilivyonavyo ndipo yakawa yanakuja maneno kama vile Mshenga,Harusi,Mahari,Baraka za Wazazi nk. Sijui wangapi tunajua majukumu haswa ya Mshenga.Anatakiwa kufanya nini, kuonana na kina nani na anahusika vipi katika mchakato mzima wa ndoa?Nafungua huo mjadala…

Sasa kwa sababu leo ni Ijumaa na sisi hapa BC tuna utaratibu wa kukumbuka na kuburudika na Zilipendwa,nikaona kwanini leo nisiweke kibao cha Mshenga Namba 1 kutoka kwao Moro Jazz wakiwa na Mbaraka Mwinshehe?Kisikilize hapo chini, burudika na uwe na wikiendi njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Tafadhali kama bado hujajiunga na Ukurasa wetu wa Facebook, nenda katika www.facebook.com/bongocelebrity ujiunge kwa kubonyeza tu kile kijisehemu cha LIKE. Au bonyeza tu juu ya hii picha hapa chini. Asante.

 

Be Sociable, Share!

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page