BongoCelebrity » Zilipendwa

“MARIAMU WANGU”-REMMY ONGALA & SUPER MATIMILA
Kwanza kabisa naomba msamaha kwa kutobandika “burudani yetu” ya zilipendwa kila ijumaa kwa takribani wiki mbili mfululizo.Nilikuwa nikibadilisha makazi kidogo.Ule mtaa niliokuwa nikikaa zamani nimehama! Ingawa haukuwa na mapaka yasiyoisha kulia lia kama alivyoimba Mwaruka katika wimbo wake Mtaa wa Saba, kuhama ilibidi.

Ni ijumaa tena.Kwa wale wanaoishi katika zile nchi zinazokuwa na majira maarufu ya “summer”, ni wakati mwingine wa kutoka nje,kuota jua na pia kutizama miili! Huu huwa ni wakati wa wazimu hususani kwa wenzetu wanaoitwa “weupe”(kuna mtu mweupe duniani?). Ukiwa na mambo ya mfadhaiko basi jikalie tu nyumbani mtu wangu.

Lakini hata sisi bongo tunayo majira yetu ya summer ingawa badala ya joto kali sisi huwa tuna kijiubaridi fulani hususani ile mikoa ya kaskazini na nyanda za juu kusini.Unajua tena,sisi tunachojali ni jina tu na wala sio hali halisi.Ukisema summer time tu kwetu inatosha.Usilete za kuleta.

Maneno pembeni,nyanyuka tucheze. Nani mwingine wa kutunyanyua vitini kucheza zaidi ya Dr.Remmy Ongala na Orchestra Matimila? Msikilize hapa akimlilia Mariamu wake katika wimbo Mariamu Wangu.Pata burudani.Wikiendi Njema.

“BINADAMU HATOSHEKI”-ORCHESTRA MAKASSY
Naam. Wikiendi tena. Wakati wa burudani. Wakati wa vikao vya kiti kirefu,familia,harusi,ubatizo,ubarikio,mwali kutolewa ndani nk.Ni muda mwingine wa kupumzisha akili.Hata kama unafanya kazi weekend hii bila shaka utakubaliana nami kwamba hata huko mabarabarani hali huwa shwari. Zile vurugu za foleni,msururu wa watu nk huwa hakuna.Ukiitazama Samora Avenue unaweza kuona kutokea Askari Monument mpaka Clock Tower.Unabisha? Hebu jaribu uone.

Kikubwa wiki hii ni kwamba tumetimiza miaka miwili. Kwa maana hiyo bado tupo kwenye mauzamauza ya kufurahi,kujipongeza na katika semina elekezi ili kuweka mstakabali wa nini kinachofuata. Kwa upande mwingine umemsikia mwenyewe mkuu wa nchi.Anasema habari za uraia wa nchi mbili hazina budi kusubiri. Anasema wasomi wamemshauri kwamba mpango wa kula huku na kule sio mzuri. Mwenyewe akasita kuleta habari za “wivu”. Wakati huo huo mkuu anasema mjenge na kuwekeza “nyumbani”. Nyumbani tena? Sijui wewe unasemaje lakini mimi naona kazi kubwa bado ipo. Washauri wasomi najua wamenielewa. Kama hawajaelewa basi tena.

Turudi kwenye burudani kwani kama ujuavyo leo ni Ijumaa. Ni mambo ya sakayonsa. Mambo ya zilipendwa. Enzi zile ambapo ugonjwa ulikuwa ni mafua tu! Wimbo unaitwa Binadamu Hatosheki kutoka kwao Orchestra Makassy. Bila shaka utakubaliana na kina Mzee Makassy.Binadamu sijui umpe nini aridhike. Hivi kwanini tupo hivyo tulivyo? Kama wanavyoimba; ukimpa jua anataka mvua. Ukimpa mvua anataka jua!Kha. Ukimpenda sana anataka kuchukiwa na ndio maana atakuletea madharau,visa,vituko na visasi.Enewei,wasikilize mwenyewe Orchestra Makassy. Pata burudani na furahia weekend yako.

Subiri kidogo. Kwa sababu wikiendi hii tunaweza kusema ni wikiendi ya BC kwa maana ya kutimiza miaka miwili sidhani kama kuna ubaya kama tukiweka kibao kingine kama zawadi….sikiliza hapo chini;

POLE MAMA- MOSE SE SENGO “FAN FAN”
Wimbo wa weekend hii nilitakiwa na ilikuwa ni dhamira yangu kuuweka hapa  wikiendi iliyopita. Sababu? Ilikuwa ni Mother’s Day kwa wengi waliopo nchi za magharibi bila kusahau kwamba siku hizi hata sisi hapa Bongo tumeshaambukizwa sijui niseme uzungu au utandawazi. Siku hizi nasi hatupitwi. Halloween tumo, Mother’s Day tumo, Father’s Day tumo,Thanksgiving tumo. Xmas na Pasaka ndio kabisa usiguse kwani hapo utachanganyikiwa nasi. Tuna barafu zetu wenyewe(pamba kwenye miti). Tuna Mbaba Xmas au ukipenda muite Father Christmas.

Sasa kwa sababu sikuuweka wikiendi iliyopita na kwa sababu kwa upande fulani naamini kwamba Mother’s Day ni kila siku, weekend hii tutajimwaya. Wimbo unaitwa Pole Mama na ni wake  Mose Se Sengo “Fan Fan” (pichani) mwanamuziki mahiri kutoka DRC ambaye alizunguka nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Tanzania(alicharaza gitaa na Makassy Orchestra). Kama ilivyo kwako wewe, katika wimbo huu Mose Se Sengo anampa pole mama yake na kumshukuru kwa yote. Nani kama mama? Pata burudani na enjoy your weekend. Kumbuka ukiamua kuiloweka,sharti uivalishe…au sio?

Shukrani: Mike Mhagama…Once a DJ,forever a DJ!

“NDOA YA MATESO”-MARIJANI RAJAB
Weekend ndio imewadia tena. Kama ulidhani wiki hii ingekuwa kavu kavu nchini Tanzania bila mikikimikiki basi ulikosea.Ilikuwa ni wiki ya “mipasho”. Ilikuwa ni rusha kombora nirushe kombora au kama vile alivyowahi kuimba Prof.Jay ukimwaga ugali mimi namwaga mboga!

Bahati nzuri ni kwamba nadhani watu wazima wamejiona ovyo na kuamua kufuata njia zinazostahili. Mchezo sasa umegeuka kuwa wa kudaiana “vijisenti”. Bila shaka umesikia mmoja kadai fidia ya Tshs Bilioni 10 huku mwingine akidai fidia ya Tsh 1 tu. Kama ingewezekana huenda angedai ile ya mkoloni kabisa iliyokuwa na tundu katikati. Sijui tugange yajayo au bado tuendelee na nguvu ya hoja,uchambuzi nk.

Tuyaache hayo.Leo ni burudani ya kale.Wenyewe mnaziita Zilipendwa. Natamani tungeziita Tunazozipenda kwani ukweli ni kwamba bado nyimbo hizi zina mafundisho kemkem na ni kama zilitungwa jana. Leo tunaye Gwiji Marijan Rajab(RIP). Wimbo unaitwa Ndoa ya Mateso. Binti karudi kwao.Anasema ndoa imemshinda.Mume anamtesa.Pesa zote anamalizia kwenye makuku ya kukaanga akiwa na “vimwana’ wake huko nje wakati familia inakufa kwa njaa.Binti hana msaada wowote,hana ndugu wala jamaa hapo alipo.Kwa masikitiko anauliza kwani kuolewa ni utumwa? Binti anaomba talaka yake.Mjumbe ndie anaombwa kuwa shahidi. Kwa uchungu na aibu anasimulia yaliyokuwa yanamsibu.Anataka kurudi nyumbani kwao kwani anasema hakuzaliwa juu ya miti bali ana kwao.Ana baba na mama. Mateso.

Pata burudani,pata ujumbe na furahia weekend yako. Maisha mafupi haya.

POLE ZA MSIBA + MEI MOSI NJEMA
Imekuwa ni wiki ngumu kwa watanzania hususani waishio jijini Dar-es-salaam na zaidi waishio maeneo ya Mbagala. Milipuko kadhaa ilitetemesha jiji.Hofu ikatanda. Ikawa mshikemshike Mbagala kwenyewe mpaka katikati ya jiji na maeneo mengine. Wengine wakajua vita nyingine labda ndio imeshawadia.Penye wengi pana mambo mengi. Maneno mitaani nayo yakazidi. Hofu ikawa hofu.

Wananchi kadhaa ambao walikuwa katika siku yao ya kawaida,ya mihangaiko ya kawaida ya maisha wakapoteza maisha. Ama kweli kifo kikija hakipigi hodi! Ndio maana tunaambiwa kila siku kwamba tujiandae. Wengi wengine wakajeruhiwa. Wengi bado wapo mahospitalini.

Vifo vinapotokea au maafa ya namna hii, huwa ni wakati wa simanzi kubwa. Kifo ni kitu cha mwisho ambacho binadamu yeyote anataka kukabiliana nacho.Kinaogopesha. Lakini kifo ni sehemu inayokwenda sambamba kabisa na maisha. Ni sehemu ya maisha na sote tutapitia njia hiyo hiyo.Tunachoweza kufanya ni kutoa pole tu kwa wote walioondokewa na wapendwa wao. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi! Pole nyingi pia ziwaendee wote waliojeruhiwa.Ni matumaini yetu kwamba Mwenyezi Mungu atawaponya na kukupeni tena afya njema.

Nini kilitokea? Ni ajali au uzembe tu wa mtu au watu fulani? Kama ni uzembe je walioathirika aidha kwa kuumia au kupoteza ndugu,jamaa na marafiki watafidiwa? Je tunavyo vitendea kazi na watendaji wa kutosha kutupatia majibu ya maswali hayo? Hayo ni baadhi ya maswali ambayo serikali ni lazima iyapatie majibu yanayoeleweka,ya wazi bila kificho. Tusipofanya hivyo,kesho bado ni tete. Yanaweza kutokea tena na tena matukio kama hili la wiki hii. Kama hali ile ilitokana na uzembe wa mtu au watu,basi hatua kali zichukuliwe. Ni wakati mwingine muafaka kwa serikali kuonyesha jinsi “inavyowajibika” kwa wapiga kura,walipa kodi na wananchi wake kwa ujumla.

Naam,kwa sababu leo ni Ijumaa na kawaida ni kwamba huwa tunaburudika na zilipendwa na kutokana na hali ya majonzi tuliyonayo,kibao cha Dr.Remmy Ongala cha Kifo ndicho ambacho nadhani ni muafaka. Kimsingi kibao hiki sio cha kuburudisha bali kutusaidia kuungana na wenzetu waliopoteza ndugu,jamaa na marafiki katika maombolezo.

Leo pia ni Mei Mosi. Ni sikukuu ya Wafanyakazi katika sehemu nyingi za ulimwenguni ikiwemo Tanzania yetu. Nachukua nafasi hii kukutakia wewe mfanyakazi na watanzania wote kwa ujumla sikukuu njema.

“NASIKITIKA”-REMMY ONGALA & MATIMILA
Mambo vipi?Nadhani nitakuwa sijachelewa sana nikikuuliza ilikuwaje pasaka yako.Ulijichana na kujirarua wapi mwenzangu?Au kutokana na hali ya uchumi ilibidi uwe mpole tu kama mwenzako hapa?

Leo sina maneno mengi.Ni Ijumaa tena na hivyo ni siku ya zilipendwa.Midundo ya leo inatoka kwa Dr.Remmy Ongala & Super Matimila Band.Wimbo unaitwa Nasikitika.

Tupende tusipende,twende mbele na kurudi nyuma, Dr.Remmy ni miongoni mwa wanamuziki ambao nyimbo zao zilikuwa zina ujumbe mkali sana.Alikuwa anaimba kama masihara hivi lakini ukweli ni kwamba ukiketi chini na kusikiliza ujumbe wake,utaupata kwa makini kabisa. Siku za karibuni nimekuwa namsikiliza sana Dr.Remmy na kwa kweli kila nikimsikiliza nasikitika kwamba mpaka hivi leo sijapata nafasi ya kufanya naye mahojiano kidogo kuhusu muziki,maisha yake na alipo hivi sasa hususani katika dunia ya “ulokole” aliyomo.One day Yes.Pata burudani,weekend njema.

CLUB RAHA LEO SHOW NA UNCLE J!
Yapo mambo ambayo ukijaribu kuyakumbuka bila shaka unaweza kutokwa na machozi.Yaweza kuwa machozi ya furaha na pia yaweza kuwa ya huzuni.Lakini kama wasemavyo walimwengu,yote huwa ni sehemu ya maisha.

Mojawapo ya mambo ambayo nikiyakumbuka huwa napata gunia la hisia tofauti tofauti ni kipindi cha Club Raha Leo Show cha enzi hizo  za Radio Tanzania Dar-es-salaam kilichokuwa kikiendeshwa na Julius Nyaisangah au maarufu kama Uncle J(pichani). Hizo ni zile enzi za utawala wa RTD kabla vituo mbalimbali vya FM havijaanza kufumuka ili kutanua wigo wa habari na mawasiliano na pia kuongeza ushindani kama sio kutuibulia pia DJs wengine ambao nao wana nafasi ya pekee katika historia ya utangazaji nchini akiwemo rafiki yangu Mike Mhagama na wengine wengi.

Kipindi cha Club Raha Leo Show kilikuwa ni sehemu muhimu sana kwa wasanii na bendi kutambulisha nyimbo zao,kukutana na mashabiki wao na pia nafasi nzuri ya wasikilizaji kutuma na kupokea salamu.Sina uhakika kama kipindi hiki bado kinaendelea.Lakini kama hakipo tena swali muhimu ni kwanini hakipo?

Kwa ijumaa ya leo burudani nzima inatoka hapo Club Raha Leo Show.Hapo utamsikia Uncle J akishirikiana na mtangazaji mwingine mahiri,Michael Katembo. Bendi iliyopo studio ni wana-Ndekule.Bila shaka kipindi hiki kitakukumbusha mbali.Natumaini utacheka kwa furaha na kama ikitokea ukalia,basi natumaini yatakuwa machozi ya furaha,

Shukrani za pekee kwa EastAfricantube na hususani mwanachama wa mtandao huo, Jphamber.Bonyeza player hapo chini uburudike.

<object width="400" height="45" data="http://www.eastafricantube.com/common/flash/music_player.swf" type="application/x-shockwave-flash"><param name="id" value="player" /><param name="align" value="middle" /><param name="allowScriptAccess" value="sameDomain" /><param name="menu" value="false" /><param name="quality" value="high" /><param name="bgcolor" value="#000000" /><param name="FlashVars" value="url=http://www.zilipendwaradio.com/files/852746240519ae36.mp3&autoplay=0&songname=CLUB RAHA LEO SHOW-JULIUS NYAISANGA" /><param name="src" value="http://www.eastafricantube.com/common/flash/music_player.swf" /><param name="name" value="player" /><param name="flashvars" value="url=http://www.zilipendwaradio.com/files/852746240519ae36.mp3&autoplay=0&songname=CLUB RAHA LEO SHOW-JULIUS NYAISANGA" /></object>

“SAMAHANI YA UONGO”-TANCUT ALMASI ORCHESTRA
Leo naomba nikiri jambo moja.Kila ifikapo Ijumaa mimi hupatwa na msisimko wa aina yake.Kwangu mimi Ijumaa ni ishara kwamba bado ningali hai na ndio naelekea kuimaliza wiki kwa maana ya mwanzo wa wikiendi.Huwa najitahidi kuitumia Ijumaa kama mwanzo mpya.Pia hupenda kuitumia Ijumaa kama mwanzo wa kutafakari yaliyojiri katika wiki nzima,kusamehe walionikosea,kuomba msamaha kwa niliowakosea,kuhakiki malengo ya mwezi/mwaka nk.Unaweza pia kuitumia Ijumaa kwa staili hiyo au ukipenda jumamosi au hata Jumapili kwa maana hiyo.

Naomba pia leo nikujulie hali.Mambo yanakwendaje?Najua hali ya uchumi bado ni tata,hauko peke yako bali tupo wengi.Cha msingi ni kwamba usikate tamaa.Endelea kupigana,endelea kuwa askari mahiri mwenye kila nia na sababu ya kushinda.Hakuna siri zaidi ya hiyo.

Leo tunao Tancut Almasi Orchestra.Wimbo unaitwa Samahani ya Uongo. Imeshawahi kukutokea mtu akakupa samahani ya uongo?Pata Burudani.Furahia wikiendi yako.

Picha kwa hisani ya Issa Michuzi.

WE STILL REMEMBER YOU!
Leo imetimia miaka 14 tangu Marijani Rajabu au “Jabali la Muziki” aiage dunia.Marijani alikuwa nyota njema ya muziki kwa miaka mingi.Aliweza kushiriki katika uimbaji na utunzi wa nyimbo nyingi ambazo zilipendwa,zinapendwa na zitaendelea kupendwa au kusikilizwa kwa miaka mingine nenda rudi.

Tunzo zake nyingi ziliweza kutamba kutokana na ukweli kwamba ziliichoma au kuigusa jamii moja kwa moja.Alitunga na kuimba kwa nyakati zilizokuwepo enzi za uhai wake na kwa wakati ujao ambao ndio huu tulio nao mimi na wewe.

Tunapomkumbuka Marijani Rajabu hivi leo tumechagua nyimbo mbili za kuendana na kumbukumbu hii.Wa kwanza unaitwa Ndoa za Mateso.Hizi bado zipo.Hivi leo kuna watu wanateseka ndani ya ndoa.Inakuwaje na kwanini?Ni vigumu sana kuelewa na pengine ndio yale wengine wanapenda kuyaita “ya dunia” huku wakimuachia anayeitwa muumba awaongoze.Hayati Marijani Rajabu aliyaona hayo,kuyatungia nyimbo na kuyaimba majukwaani.Leo tunamkumbuka.

Ukisikiliza sana nyimbo za siku hizi utagundua jambo moja.Ni chache sana zinazogusia hali halisi ya siasa au uchumi achilia mbali sehemu zingine za jamii zaidi ya mapenzi. Leo hii karibuni kila wimbo unaotoka ni kuhusu mapenzi,kutamaniana,kuumizana kimapenzi nk.Sehemu zingine za jamii(ambazo naamini ni muhimu pia) zimesahauliwa. Jabali la Muziki yeye hakuwa hivyo.Aligusia karibuni kila kona.Pengine ndio maana,pamoja na kutoweka kwake miaka 14 iliyopita,anabakia kuwa “Jabali”.Wimbo wa pili ni uthibitisho wa ninachokiongelea hapo juu.Unaitwa  Dunia Uwanja wa Fujo.Hili sidhani kama linahitaji mjadala mwingi kwani ni wazi kwamba dunia ni uwanja wa fujo.Sikiliza kwa makini nyimbo zake kisha tusaidiane kujiuliza swali zuri; Nani mrithi wake miongoni mwa wanamuziki wa leo?

Endelea kupumzika kwa amani Marijani.We still remember you!

Special Thanks: www.changamotoyetu.blogspot.com

TANZANIA RHYTHM-RTD(MIKIDADI MAHMOUD)
Bisha shaka ushasikia watu wakisema Cha Kale ni Dhahabu. Kwa wale wanaotumia lugha ya malikia wanasema Old is Gold. Nadhani ya kale huwa yanageuka kuwa dhahabu kwa sababu ya kale ni historia.Sasa kama tujuavyo,historia ndio msingi wa kujua unapokwenda. Mwanafalsafa fulani aliwahi kuweka bayana kabisa kwa kusema mtu asiyejua historia yake ni kama “mtu mfu’.Hakukosea.

Hapo zamani kidogo Bongo yetu haikuwa na vituo vya redio vya FM.Hapakuwa na vituo vya televisheni tunavyovyiona hivi leo.Ukitaka burudani au kusikia taarifa ya habari(mara nyingi ikiwa sensored) ulikuwa huna budi ku-tune on Radio Tanzania.RTD ndio ilikuwa yetu.Zile zilikuwa enzi za radio za philips na betri za national.Ni enzi za…..unaweza kuongezea list.

Enzi hizo zilikuwa na watangazaji kama Mikidadi Mahmoud(pichani).Leo hii utamsikia akiturudisha enzi zileeee.Kipindi kilikuwa kinaitwa Tanzania Rhythm kupitia External Service ya RTD.Utundu huu sijui kaufanya nani lakini mimi nimeufuma pale EastAfricantube.Kuna sehemu ya kwanza na ya pili.Pata burudani na weekend njema.