BongoCelebrity

SHUHUDIA FAINALI YA KOMBE LA UEFA JUMAMOSI HII KUPITIA DStv
Jumamosi imekaribia. Mashabiki wa soka duniani wanalo la kuzungumzia, kujadili na kisha siku ya siku kujumuika kwa pamoja kushuhudia mechi kali na ya aina yake. Ni fainali ya Kombe la UEFA baina ya timu mbili kutoka Ujerumani Bayern Munich wakipambana na Borussia Dortmund.

Fainali hii ambayo itafanyikia jijini London nchini Uingereza katika uwanja maarufu wa Wembley, inazikutanisha timu mbili kutoka Ujerumani ambazo zilitinga fainali hiyo baada ya kuiangusha miamba ya soka toka Hispania, Real Madrid na Barcelona. Real Madrid walipokea kipigo cha 3-1 nchini Ujerumani na ingawa katika mechi ya marudiano Real Madrid walishinda bao 2-0, Borrusia Dortmund wakasonga mbele.

Kwa upande wa Bayern Munich wao waliingia kwa kishindo zaidi baada ya kuwachapa Barcelona jumla ya bao 4-0 katika mechi ya kwanza na 3-0 katika marudiano pale Nou Camp.

Je,ni nani ataibuka mshindi katika fainali hii? Ni Bayern Munich au Borussia Dortmund? Usikose kutizama kipute hiki kupitia DStv pekee!

NITOKEJE?

“KAMA ZAMANI”-MwanaFA Feat. THE KILIMANJARO BAND, MANDOJO & DOMOKAYA (BrAnD NeW)
Huu wimbo ulitoka rasmi wiki iliyopita. Kwa makusudi sikuuweka hewani. Nilikuwa na bado nina maana yangu. Ukiendelea kusoma bila shaka utanielewa.

Kila kizazi kina tabia au haki ya kudai kwamba muziki wao, wa enzi zao, ni bora kuliko wa kizazi kingine. Bila shaka hilo halikushangazi. Ulitegemea kizazi fulani kiseme kwamba chao kilikuwa au ni cha mbumbumbu wasio wabunifu wala wenye kuchangamsha akili zao na kutengeneza vitu vya nadra?! Sidhani….mwamba ngoma huvutia upande wake. Ni hulka ya binadamu.

Lakini historia ya binadamu inaonyesha kwamba mahali ambapo binadamu alifanya vyema zaidi ni pale aliposhirikiana na wenzake.Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Bila shaka kuna kila aina ya ukweli katika hili.

Kwenye sanaa ya muziki nchini Tanzania, miongoni mwa wasanii ambao wameamua kwa makusudi kuileta dhana hiyo kwa vitendo ni MwanaFA. Yeye(na nakubaliana naye kabisa) anaamini kwamba kila kizazi kina yake mazuri. Cha msingi ni kuendeleza yale mazuri na kuachana na yale ambayo hayana maana. Kuna muziki mzuri kutoka kizazi kile. Kuna muziki mzuri kutoka kizazi hiki.Kwanini tusichanganye tukapata kizuri zaidi? Ameeita kampeni yake Keeping The Good Music Alive.

Hicho ndicho alichokizangatia alipotoka na Yalaiti ikiwa ni maingiliano ya enzi zile za Sitti Binti Saad na sasa. Linah akaingia na kukoleza ya kale na mapya. Huu hapa sasa ni ujio wake katika wimbo Kama Zamani akiwa amewashirikisha The Kilimanjaro Band (Njenje) na Mandojo & Domokaya.

Sasa kwanini nimesubiri mpaka leo kuweka post hii? Ni hivi; naunga mkono harakati hizi za MwanaFa za Keeping The Good Music Alive. Niliona kwa sababu naunga mkono juhudi hizi, basi nisubiri kwanza kibao hicho kipatikane kwenye platforms mbalimbali za mtandaoni ambapo na wewe unaweza kuunga mkono jitihada zake kwa kuununua copy yako.Usikilize hapa chini…lakini kama unaamini kwamba muziki mzuri unahitaji maandalizi mengi na yenye kugharimu, basi tafadhali ungana nami katika juhudi za kuwasaidia wasanii wetu(akiwemo MwanaFA) kwa kununua kazi yake.

Naam unaweza kununua wimbo huu kwa kufuata Links hizi.Kumbuka ORIGINALS ARE MASTERPIECES.Let’s support our artists(especially those who makes good music). Nunua kupitia Links Zifuatazo;

KUNUNUA KUPITIA AMAZON BONYEZA HAPA

WASANII KUTOKA NIGERIA, KENYA NA AFRIKA KUSINI KUPAMBA UZINDUZI WA BIG BROTHER AFRICA-THE CHASE
Wasanii mbalimbali kutoka Nigeria, Kenya na Afrika Kusini wanatarajiwa kupamba shughuli ya kuanza kwa msimu mpya wa show kabambe ya Big Brother Africa siku ya Jumapili tarehe 26 May.Show ya msimu huu imepewa jina la The Chase. Jumla ya washiriki 28 ambao wamechaguliwa kushiriki show ya mwaka huu watatambulishwa rasmi  siku hiyo katika tukio ambalo linatarajiwa kuonyeshwa “Live” katika nchi zizizopungua 50.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, tukio hilo litaanza kuonyeshwa saa moja jioni kwa saa za Afrika ya Kati (19:00 CAT) katika AfricaMagic, AfricaMagic Entertainment, AfricaMagic World na pia kwenye channel 197 na 198 katika DStv.

Msanii kutoka nchini Kenya,STL anayetamba na vibao vyake kama vile “Take My Time” , “Hula Hoop“, “Bad as I Wanna Be“, mshindi wa tuzo za Kisima, Clops na Jeermaan ameahidi kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki wa muziki na hususani mashabiki wa Big Brother Africa.

Taarifa hiyo inazidi kupasha kwamba kutoka nchini Nigeria, wasanii Don Jazzy, D’ Prince n’ Wande Coal wanatarajiwa kuwakamata vilivyo mashabiki. Don Jazzy, mshindi wa tuzo mbalimbali kama prodyuza, mwimbaji na mwandishi na mwanamuziki atakuwa bega kwa bega D’ Prince na Wande Coal wakitumbuiza na vibao vyao kama vile “I like What I See”, “Bumper 2 Bumper” na “Who Born the Maga”.

Kisha kundi maarufu la muziki wa Afro Pop kutoka Afrika Kusini la Mafikizolo linatarajiwa kuwa kivutio cha kipekee wakati za uzinduzi huo. Kundi hilo ambalo mpaka sasa limeshaweka kibindoni tuzo mbalimbali linatarajiwa kuteka mashabiki kwa nyimbo zao kama vile ”Sibongile”, “Ndihamba Nawe”, “Nisixoshelani” na “Khona”.

Pia katika kuongeza orodha ya watoaji burudani katika usiku huo, mchekeshaji Daniel Ndambuki, maarufu zaidi Churchill kutoka nchini Kenya kuwavunja mbavu watazamani na wahudhuriaji wa uzinduzi huo. Churchill amejipatia umaarufu kutokana na TV show yake inayokwenda kwa jina “Churchill Live”.

Taarifa iliyotolewa inamalizia kwa kubainisha kwamba kwa mashabiki ambao kwa sababu moja au nyingine watashindwa kutizama uzinduzi huo kupitia kwenye luninga zao, habari njema ni kwamba wanaweza pia kutizama kupitia mtandaoni kwenye  www.bigbrotherafrica.com.

Baada ya uzinduzi huo unaotarajiwa kuwa wa kufana kitakachofuata ni siku 91 za kutizama kinachoendelea ndani ya Big Brother Africa kupitia channel 197 na 198.

“SHANNI NA JENNY”-ABBY SKILLS Feat.CHEGE
Ni muda kidogo hatujasikia kitu kutoka kwa Abby Skills ambaye kwa watu wanaokumbuka enzi zile Bongo Fleva inaanza kushika kasi, mtamkumbuka vizuri. Huu hapa ni wimbo wake mpya akiwa amemshirikisha Chege. Wimbo unaitwa Shanni na Jenny. Msikilize

BREAKING NEWS: PROFESSOR JAY AJIUNGA NA CHADEMA/ AKABIDHIWA KADI YA UANACHAMA DODOMA
Pichani Professor Jay akiwa na Kiboya,mdau mkubwa wa muziki nchini ambaye pia ni mwanachama wa CHADEMA. Picha kwa hisani ya Twitter ya Professor.

Habari ambazo zinatambaa hivi sasa mtandaoni ni kwamba msanii maarufu na miongoni mwa wanaoaminika kuwa waasisi wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Professor Jay (jina halisi Joseph Haule), amejiunga rasmi na harakati za siasa nchini kwa kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Professor Jay ambaye tungo zake mara kwa mara zimekuwa zikijikita katika kutetea maslahi ya wananchi, amejiunga na CHADEMA huko Dodoma ambapo amekabidhiwa rasmi kadi ya uanachama.

Zoezi hilo limesimamiwa na John Mnyika, Mbunge wa Ubungo na Joseph Mbilinyi (Sugu) Mbunge wa Mbeya Mjini na kushuhudiwa na wanachama wengine kadhaa ambao aidha ni wanamuziki pia au wadau wa karibu wa muziki.

Bila shaka kujiunga kwa Professor Jay na CHADEMA kunaashiria kwamba yupo mbioni kugombea Ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Professor Jay ni mwenyeji wa Mikumi-Morogoro na hivyo haitoshangaza kama ataamua kugombea katika jimbo hilo hapo mwaka 2015.

Professor Jay akikabidhiwa kadi na Mh.Joseph Mbilinyi.

BILLBOARD MUSIC AWARDS: JUSTIN BIEBER AZOMEWA/ MIGUEL APIGA MWELEKA
Yawezekana hukupata nafasi ya kuangalia baadhi ya mambo yaliyojiri jana wakati wa Billboard Music Awards ambazo zilitangazwa kutokea Las Vegas,Nevada-mji wa kila aina ya dhambi ambapo unaambiwa unachokiona au kukikuta pale kiachie hapo hapo.

Miongoni mwa yale yaliyojiri ni pamoja na msanii Justin Bieber kuzomewa na Miguel kupiga mueleka. Bieber amezomewa baada ya kuonekana akijifaragua kupita kiasi wakati akipokea Tuzo. Katika siku za hivi karibuni, Justin Bieber ambaye ni mzaliwa wa nchini Canada mwenye miaka 19, amekuwa akipamba kurasa za mbele za magazeti na vyombo vingine vya habari kwa sababu ambazo hazipendezi.

Kwa Miguel yeye ni ajali ambayo bila shaka atakuja siku kusema It was the most embarrassing moment of his career. TIZAMA HIZI VIDEO

JUSTIN BIEBER AZOMEWA

MIGUEL APIKA MWELEKA

KINACHOMPONZA PRODYUZA TUDD THOMAS NI UCHAWI AU KUSAHAU?
Prodyuza Tudd Thomas.

MASHABIKI wa mtayarishaji wa muziki (Producer), mwenye uwezo wa kipekee, aliyetayarisha wimbo wa Leka dutigite wa Kigoma All Stars na zingine nyingi, Tudd Thomas, wamekuwa wakiulizana maswali mengi wao kwa wao pasipo kupata majibu.

Safari ya Tudd Thomas katika muziki, ilianzia mkoani Iringa akiwa Iringa Records aliporekodi wimbo wa mwanamuziki Marlaw unaoitwa Bembeleza. Wimbo huo ulipata tuzo ya wimbo bora wa mwaka kutoka Kilimanjaro Tanzania Music Awards mwaka 2008 na pia kumfanya Marlaw apate tuzo ya msanii bora wa kiume kupitia tuzo hizo. Baadae alihamia jijini Dar es Salaam na ndipo alipoonesha uwezo wake zaidi kwa kusuka nyimbo zilizotikisa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Hakuna asiyeufahamu wimbo wa Pii Pii (Missing my baby) wa Marlaw ambao aliutengeneza yeye kupitia Studio ya JML. Wimbo huo ulipata tuzo nyingi ikiwa ni pamoja na tuzo ya Nzumari nchini Kenya mwaka 2009 mbapo uliingia kwenye kipengere cha wimbo bora wa Afrika Mashariki, kumfanya Marlaw aingie kwenye kipengele cha msanii bora wa Afrika Mashariki na kunyakua tuzo hiyo. Baada ya hapo wimbo huo ulipata tuzo ya Kilimanjaro nchini Tanzania kama wimbo bora wa mwaka wa Afro pop mwaka 2010, tuzo ya Chaguo la Teneez Music nchini Kenya kama wimbo ulioongoza kwa kuchukuliwa kwa njia ya mtandao Afrika Mashariki “The most downloaded East African song” mwaka 2010, pamoja na tuzo ya Nigeria Sound City Video Music kama wimbo bora wa Afrika Mashariki mwaka 2010.

Aliendelea kutayarisha nyimbo ambazo zilipata umaarufu mkubwa na kuingia kwenye vipengele mbalimbali vya tuzo za muziki za Kilimanjaro. Mwaka 2012, nyimbo tatu zilizotokana na mikono yake zilipata nafasi ya kushiriki tuzo hizo. Nyimbo hizo ni Liz One wa Izzo Business ambao uliingia kwenye vipengele viwili ambavyo ni wimbo bora wa mwaka na wimbo bora wa Hip hop na pia kusababisha msanii huyo aingie kwenye kipengele cha msanii bora wa Hip hop. Milele daima wa Barnaba na Kizunguzungu wa Rachel, ambapo zote ziliingia kipengele cha wimbo bora wa Zouk/Rhumba pia ni nyimbo alizotengeneza mtayarishaji huyo.

Nyimbo zingine alizotayarisha ambazo zilifanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na TV ni Kisa pombe na Soldier za Mwasiti, Sorry sana, Mbayuwayu na Mtoto wa Afrika za Marlaw pamoja na Natumaini ya Becka aliyowashirikisha Barnaba na Amin. Pia zipo nyingine kama Unikimbie ya Amin, Tushukuru kwa yote ya Ditto, Lonely ya Linah na Magubegube ya Barnaba.

Mtayarishaji huyo ambaye hajawai kuingia kwenye tuzo za Kilimanjaro za muziki wa hapa nchini Tanzania ambazo mwaka huu zimeongezewa kipengele cha Mtayarishaji bora chipukizi ndiye aliyetayarisha wimbo wa Leka dutigite wa Kigoma All Stars kupitia Studio yake ya Ngoma Records. Wimbo huu umeingia kwenye kipengele cha wimbo bora wa mwaka 2013. Pia alishirikiana na mtayarishaji Imma the boy kutengeneza wimbo wa Me ‘n’ U wa Ommy Dimpoz ambao umeingia kwenye kipengele hicho na vipengele vingine ambavyo ni wimbo bora wa Bongo Pop na wimbo bora wa kushirikiana.

Alipoulizwa alisema hapendi kuzungumzia juu ya kutotajwa kama miongoni mwa wanaowania tuzo. Aliendelea kusema kwamba, hata kama baadae ikitokea, kwake ni motisha tu, lakini kikubwa zaidi ni kwamba anahisi analo deni kubwa la kutumia uwezo wake ipasavyo kufanya kazi nzuri zaidi ya hapo ili kuutangaza muziki wa Tanzania kimataifa. Pia alisema ana malengo makubwa aliyojiwekea na ndiyo maana kila kukicha anawaza kutayarisha nyimbo zenye tofauti na zenye radha ya kipekee.

Tudd Thomas anaendelea kukitumia kipaji chake na ujuzi wake ipasavyo na siku chache zilizopita kuna nyimbo zisizopungua tatu zilizoingia sokoni na zinafanya vizuri, ambazo ni kazi za mikono yake. Nyimbo hizo ni Uswazi take away ya Chegge, Nyumbani ya Kigoma All Stars na pia ameshirikiana kwa kiasi kikubwa na mtayarishaji Fundi Samwel kutengeneza wimbo wa Mahakama ya mapenzi wa Linex.

“NASHINDWA KULALA”- BONFACE MATEZA
Huu hapa ni wimbo mpya kutoka kwa msanii Bonface Mateza.

MSANII   :  BONFACE MATEZA

WIMBO   :  NASHINDWA KULALA

STUDIO  :   JAIM RECORD

PRODUCER  :  GEORGE   JAMES

YANGA YAICHAPA SIMBA 2-0/ MASHABIKI BARANI AFRIKA WAFURAHIA MECHI KUPITIA SuperSport EAST 9
Yanga wakifurahia mojawapo ya magoli kutoka katika mechi hiyo. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry Blog

Timu ya soka ya Yanga, jioni hii imewadhihirishia mashabiki wao na wapenzi wa soka barani Afrika kwamba msimu huu ulikuwa wao baada ya kuwachapa wapinzani wao wa jadi,Simba kwa jumla ya magoli 2-0 katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mchezo ambao ulionyeshwa kote barani Afrika kupitia SuperSport East 9 ndani ya DStv.

Mashabiki wa soka nchini Tanzania na barani Afrika waliweza kuona mpambano huu wa watani wa jadi Live kupitia kwenye luninga zao kwenye  SuperSport 9 East ambao walirusha matangazo hayo moja kwa moja kutokea Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo magoli ya Yanga yalifungwa na Didier Kavumbagu kunako dakika ya 5 ya kipindi cha kwanza na Hamis “Diego” Kiiza kunako dakika ya 63 ya kipindi cha pili.

Kwa matokeo hayo, Yanga inamaliza msimu wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 60, ikifuatiwa na Azam FC yenye 52 na Simba 45.Hii ni mara ya 24 kwa Yanga kutwaa taji la Ubingwa wa Soka Tanzania Bara. Hongera kwa Yanga!