Lipo kundi la wasanii ambao kwa makusudi wao wamejikita katika kuimba nyimbo za mapenzi.Sajna ni mmojawapo miongoni mwa wasanii hao.Yeye,kama ilivyo kwa kina C-Madini na wenzake,ni uzao au chimbuko kutoka Tetemesha Records kule Mwanza.
Ninaposema amejikita katika kuimba nyimbo za mahaba au mapenzi,sina maana mbaya.Anaweza.Ni vizuri kufanya kile ukipendacho na ukiwezacho.Ni siri ya mafanikio kama vile mazoezi na michezo.Huu hapa chini ni wimbo mpya kutoka kwake.Unaitwa Mbalamwezi.Ni hadithi nyingine nzuri ya kimapenzi.Usikilize
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Mwimbaji na muigizaji maarufu kutoka nchini Marekani,Whitney Houston,amefariki dunia muda mfupi uliopita(Jumamosi mchana saa tisa na dakika hamsini na tano kwa saa za Marekani-Pacific) akiwa na umri wa miaka 48. Whitney Houston ambaye ni miongoni mwa waimbaji waliokuwa na kipaji cha aina yake katika uimbaji,amekutwa na walinzi wake wa karibu(bodyguards) akiwa hajitambui katika gorofa ya nne ya chumba cha hotel ya The Beverly Hilton alipokuwa amefikia. Watu wa dharura walijaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio na hivyo ikatangazwa rasmi kwamba amefariki.
Whitney ambaye alikuwa na kipaji cha aina yake katika uimbaji,amefariki dunia katika mkesha wa tuzo maarufu za Grammy na alikuwa amepangwa kutoa burudani katika party ya Clive Davis,producer na music mogul ambaye amekuwa na Whitney Houston tangu alipoanza muziki.
Kwa muda mrefu,Whitney Houston, ambaye aliwahi kuolewa na mwanamuziki mwingine maarufu,Bobby Brown(walizaa mtoto mmoja Bobbi-Kristina Brown baada ya kuoana mwaka 1992 na kuachana mwaka 2007) amekuwa na tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya.Aliwahi kutunukiwa Udaktari wa Heshima kutoka Granning State University cha huko Lousiana.
Huu hapa ni miongoni mwa wimbo kutoka kwake ambao binafsi naupenda sana
PUMZIKA KWA AMANI WHITNEY!
Mpaka hivi sasa inakadiriwa kwamba mtandao wa Facebook una zaidi ya watumiaji milioni 845.Idadi ya namna hiyo ndio ulioufanya mtandao huo kuorodheshwa katika masoko ya hisa duniani na hivyo kuwapa watu wengi zaidi nafasi ya kuwekeza!
Sasa ili kuonyesha ni jinsi gani mtandao huo upo makini na unasoma na kusikiliza karibuni kila kitu tunachobwabwaja ndani yake, hapo jana mtandao huo umetoa orodha ya nyimbo ambazo hupigwa zaidi pale watu wanapoanza mahusiano ya kimapenzi na pale mapenzi yanapofikia kikomo au kwa lugha ya mtaani “wapenzi wanapomwagana”.Endapo unashangaa ni wapi Facebook wanapata data kama hizo,jibu ni kwamba kila kukicha watu wapo bize kuiambia Facebook kupitia Status zao. Sikutaki tena,Jamani Nampenda,Anantia raha,ananiudhi nk ni baadhi tu ya status ambazo zinaweza kuelezea mengi.
Kupitia huduma ya Facebook ya Status na Nyimbo Unazozisikiliza, mtandao huo unaona wazi kinachoendelea na hivyo kupitia data hizo hizo,wameweza kupata orodha ya nyimbo maarufu katika mafungu hayo mawili ya mapenzi yaani Yanapoanza na Yanapokwisha,
Wimbo ambao umeonekana kupendwa zaidi na watu wanapoanza mapenzi ni ule wa Don’t Wanna Go Home wa Jason Derulo wakati wimbo unaoitwa The Cave wa Mumford & Sons umeonekana kukolea zaidi wapenzi wanaitimisha safari yao ya mapenzi.
Hii hapa ni orodha kamili ya nyimbo hizo.Ukizingatia kwamba Jumanne ijayo ni siku ya Wapendanao yaani (Valentine’s Day) siku ambayo ni maarufu kwa aidha mapenzi yanayoanza au yanayofikia ukingoni.
Hizi hapa ni Nyimbo Maarufu Kwa Wapenzi Wanaoanza Safari Yao Ya Mapenzi;
“Don’t Wanna Go Home” by Jason Derulo
“Love on Top” by Beyoncé
“How to Love” by Lil Wayne
“Just the Way You Are” by Bruno Mars
“Good Feeling” by Flo Rida
“It Girl” by Jason Derulo
“Stereo Hearts” by Gym Class Heroes featuring Adam Levine
“Criminal” by Britney Spears
“No Sleep” by Wiz Khalifa
“Free Fallin’” by John Mayer
Hizi Hapa Ndio Zile Maarufu Mapenzi Yanapogeuka Kuwa Machungu Kama Shubili
“The Cave” by Mumford and Sons
“Crew Love” by Drake
“All of the Lights” by Kanye West
“Rolling in the Deep” by Adele
“Take Care” by Drake
“It Will Rain” by Bruno Mars
“We Found Love” by Rihanna & Calvin Harris
“Call It What You Want” by Foster the People
“Love You Like a Love Song” by Selena Gomez and the Scene
“Without You” by David Guetta featuring Usher
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla,Rose Muhando(pichani), hapo jana imewekwa wazi kwamba ameingia mkataba mnono na kampuni mahiri katika masuala ya muziki na burudani hapa ulimwenguni,Sony Music.
Rose Muhando ambaye anakuwa msanii wa kwanza wa muziki wa injili nchini Tanzania kuingia mkataba wa namna hiyo na Sony Music,atasimamiwa kutoa album tano hiyo ikiwa ni katika suala zima la uandaaji na usambazaji.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Biashara wa Sony Music,Russell Crawford,kampuni yake imedhamiria katika kuwawezesha wasanii wa hapa nyumbani kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa wasanii mbalimbali duniani ikiwemo wale maarufu kama vile Usher, Chris Brown, Toya Delazy, Beyonce, Pitbull, Tumi and the Volume, J Cole and R Kelly.
BC inapenda kutoka pongezi nyingi kwa Rose Muhando na timu yake yote.
Photo Credit:Global Publisherz
Recently,Tanzania’s renowned Fashion Designer,Mustafa Hassanali,had a chance to showcase his unique talent at the Bangalore Fashion Week 2012 that was held in India.Here are some of the images and what Mustafa brought to the Runway.
A model wearing one of Mustafa Hassanali’s design during Bangalore Fashion Week 2012
A model wearing one of Mustafa Hassanali’s design during Bangalore Fashion Week 2012
A model wearing one of Mustafa Hassanali’s design during Bangalore Fashion Week 2012
Mustafa Hassanali during grand finale with showstopper Tanzania model based in sweden Michel Jeng
Kuna habari kwamba “bifu” linalojitokeza mara kwa mara ndani ya Bunge (na wakati mwingine kuhamia katika mtandao jamii wa Facebook) kati ya Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dr.Emmanuel Nchimbi na Waziri Kivuli wa Wizara hiyo,Mbunge wa Mbeya Mjini(CHADEMA),Joseph Mbilinyi almaarufu kama Sugu,sio la ndani ya Bunge tu bali hata wawapo nje ya mjengo huo ambapo sheria zote za nchi hutungwa.
Lakini pamoja na kuwepo kwa tetesi hizo,katika siku za hivi karibuni wawakilishi hao wa wananchi wameonekana kutokuwa na tofauti za “kihivyo” wanapokuwa nje ya Bunge kama picha ya hapo juu inavyoonyesha kitu ambacho kinatufanya tujiulize kama tetesi hizo zina ukweli au ni watu tu wanataka jamaa waingie katika mgogoro binafsi badala ya kuendelea kupambana katika masuala ya sera na kazi.
Familia ya Ndugu Abdallah Mrisho Salawi – Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, inachukua fursa hii kutoa shukrani za dhati kwa watu wote walioshiriki, kwa namna moja au nyingine, katika mazishi na maziko ya mpendwa mkewe, Khadija Abdulhussien, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Alhamis Feb 2, 2012, katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam.
Shukrani za pekee ziwaendee wafanyakazi wote wa Global Publishers na hususani Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Eric Shigongo, ambaye alikuwa akifuatilia kwa karibu maendeleo ya afya ya marehemu tangu mwanzo na kutoa ushauri kila mara, alijitolea kwa hali na mali ili kuokoa maisha ya mpendwa wetu bila kuchoka hadi dakika ya mwisho neno la Mungu lilipotimia.
Shukrani pia ziwaendee Dk. Wayi wa Kinondoni Hospital, Dk. Hirji wa Ebrahim Hajji Hospital na Dk. Nyawawa wa Aga Khan Hospital kwa jitihadi walizozifanya za kujaribu kuokoa maisha ya Khadija.
Familia inawashukuru pia majirani, jamaa na marafiki wote wa Mrisho waliyoko nchini na nje ya nchi ambao wamekuwa wakimfariji kwa njia mbalimbali za mawasiliano na kumtia moyo katika kipindi hiki kigumu.
Familia haina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mungu abariki kila jambo mnalolifanya hapa duniani na hakika mmejiwekea thawabu nyingi kwake. Kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti, basi hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutimiza ahadi yake na tuseme: Yeye (khadija) ni wa Mwenyezimungu na kwake Mungu sote tutarejea!
Mungu ampumzishe Khadija katika moja ya viwanja vya peponi – Amen!
Hakuna ubishi kwamba wimbo wa KamiliGado kutoka kwa Professor Jay akiwa amemshirikisha Producer maarufu,Marco Chali,ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vizuri sana katika mzunguko wa nyimbo za Bongo Fleva iwe ni katika radio,mtaani,club na katika miito ya simu yaani ringtones nk.
Sasa habari zilizopo mtaani ni kwamba The Heavy Weight MC,yupo mbioni kuiweka video ya KamiliGado katika luninga hivi karibuni baada ya maandalizi ya mpango huo mzima kukamilika.Habari hizo pia zinapasha kwamba Professor Jay atakuwa msanii wa kwanza kushoot video yake kwa kutumia vifaa vya kisasa kabisa ambavyo kampuni ya Visual Lab(Next Level) inayoongozwa na Adam Juma,imevipata hivi karibuni.Kwa maana hiyo,video ya KamiliGado huenda ikawa katika kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika video za wasanii wengine hapa Bongo.
Siku chache zijazo,msanii Steve Nyerere,ambaye yaelekea ameamua kujikita katika filamu zenye uhalisia fulani hususani zenye mrengo wa kisiasa,anatarajiwa kuzindua filamu yake mpya inayokwenda kwa jina Respect Nyerere ikiwa ni filamu kuhusu baadhi ya matukio au mambo yatokanayo na maisha ya Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Steve Nyerere ambaye hivi karibuni alitoa filamu ya Mr.President ambayo ni filamu yenye matukio sambamba na maisha ya Rais wa sasa,Jakaya Mrisho Kikwete,amesema filamu ya Respect Nyerere itazinduliwa rasmi tarehe 14 Februari 2012 katika Hotel ya Serena jijini Dar-es-salaam.


sending...








